MTENDAJI ATUHUMIWA KUNYANYASA FAMILIA
MTENDAJI
wa kata ya Usa river wilayani Arumeru, John Laizer anatuhumiwa kuinyanyasa familia moja na kuisababisha kuishi kwenye
mazingira magumu ya hofu ambayo yanatishia usalama na uhai wao na kuzuia
uendelezaji wa nyumba inayojengwa kwa ajili ya familia hiyo ya mama na watoto
wake wawili.
Kwa
mujibu wa mmoja wa familia hiyo,Ephata Abrahamu Swai, mkazi wa kijiji cha Emanyata,
amewaambia wanahabari kijijini hapo kwamba Mtendaji huyo amekuwa akitumia
madaraka yake vibaya kwa kutaka aabudiwe kama mungu mtu kuzuia familia hiyo isiweze kuendeleza nyumba
inayojengwa na ndugu zake na mwanamke kwa ajili ya familia hiyo bila ridhaa yake.
Ephata,
amemtuhumu kaka mkubwa wa familia hiyo ya Swai,aitwae Simion Abraham Swai,
ambae pia ni ni mzee wa Kanisa la AMEC, kwa kushirikiana na mtendaji huyo
kuchochea mgogoro , kwa kuwa alitaka kuuza eneo la mdogo wake aitwae
Joseph Abraham Swai, analoishi na mkewe ,ambae kwa sasa yuko mahabusu
akikabiliwa na tuhuma za kesi ya mauaji .
Ephata
,amesema kabla ya mdogo wao kupatwa na mkasa wa kutiwa mbaroni alikuwa akiishi na
mke wake aitwae Anande (40) ambae wamezaa nae watoto wawili mmoja wa kiume
aitwae Emanuel na mwingine wa kike aiwae Jesca.
Alisema
kuwa katika mgogoro huo ndugu wote sita wa familia hiyo na ndugu wa koo wapatao
30 ,walikaa katika kikao kilichofanyika Juni 20 mwaka huu na kukataa kuuzwa kwa
eneo hilo ,na badala yake walikubaliana ndugu zake mwanamke waendelee na ujenzi
wa nyumba hiyo lakini ilipofika Juni 10 walipokea amri toka kwa Mtendaji wa
Kata hiyo akizuia ujenzi huo bila ufafanuzi zaidi.
Ephata,amesema
walifikisha swala hilo ofisini kwa mtendaji wa Kata na pamoja na maamuzi
ya kikao cha ukoo ambayo yaliruhusu ujenzi kuendelea na mtendaji huyo
aliyaafiki na baada ya muda wa wiki moja mtendaji kupitia kwa Mwenyekiti
wa Kitongoji aitwae Jeremia Abel Urio, walipokea amri ya kuzuia tena ujenzio
usiendelee bila ufafanuzi .
Wameshangazwa
kuona mtendaji anakuwa ni kikwazo na kutokana na maagizo yake anayoyatoa
kupitia njia ya simu ya mkononi,kwa mwenyekiti wa Kitongoji, kuzuia eneo hilo
lisiendelezwe kitendo ambacho ni matumizi mabaya ya madaraka yake kwa kuwa
anasababisha migogoro katika familia na jamii .
Mtendaji
huyo, alipotakiwa kutoa ufafanuzi juu ya
sakata hilo alidai kuwa yeye alitumia mamlaka ya kuzuia ujenzi huo ili kupata
mwafaka wa wanafamilia hao,hata hivyo alishindwa kufafanua iwapo amefanikiwa
kumalizika kwa mgogoro .
Ephata
amesema tayari kilio chao hicho wameshakifikisha kwaMkuu wa wilaya ya Arumeru,
Deus Mnasa Sabhi, kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi wa mgogoro huo ili kuwezesha
familia hiyo kundeleza eneo lao,hata hivyo mkuu huyo ameahidi kushughulikia
suala hilo.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia