MFANYABIASHARA ASHIKILIWA KWA KUMUOA MTOTO WA MIAKA 8 NA KUMPA MIMBA

MFANYABIASHARA aliyetambulika kwa jina la Joseph Ngisha(24)mkazi wa
sakina ,Songambele,jijini Arusha anashikiliwa na polisi kwa kosa la
kumuoa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8 kinyume cha sheria kwa
mahari ya ngómbe 4.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Arusha,Liberatus Sabas ,polisi
pia inamshikilia baba mzazi wa mtoto huyo,Lemomomo Olokuto(42)mkazi wa
Mto wa mbu kwa tuhuma za kumwoza mtoto wake tangu mwaka 2010 ,ambapo
sasa ana umri wa miaka 11.

Alisema Ngisha alitiwa mbaroni julai 18 mwaka huu majira ya saa 3.45
asubuhi nyumbani kwake baada polisi kupata taarifa za siriki na
kumkuta akiishi na mtoto huyo huku akiwa amembebesha ujauzito wenye
umri wa miazi mitatu.

''Ngisha alipohojiwa na polisi alikiri na kueleza kuwa yeye alitoa
mahari ya ngómbe 4 badala ya 3 zinazotajwa na baba mkwe wake''alisema

Kamanda Sabas alifafanua kuwa Ngisha alianza kumchumbia mtoto huyo
baada ya kuacha  kunyonya kwa mama yake na kwamba alipofikisha umri
huo aliwafuata wazazi wake na kuwaeleza nia ya kutaka kumchumbia.

Hata hivyo mzazi wa upande wa mama  aligoma huku baba yake ambaye ni
mtuhumiwa akiruhusu mtoto wake aolewe bila kupingwa.

Aliongeza kuwa mtuhumiwa Ngisha baada ya kuona mama mzazi akipinga
mtoto wake asiolewe, alimrubuni  kuwa anakwenda kumsomesha shule
,kitendo ambacho hakukifanya na badala yake alikuwa akimwingilia
kimapenzi na kumfanya kama mke .

Kamanda alisema  kuwa taarifa za mtuhumiwa kuishi na mtoto huyo kama
mke ziligunduliwa na majirani kwani mara nyingi alikuwa akimfungia
ndani bila mtu kujua huku akiwaeleza baadhi ya jamaa zake kuwa ni
mdogo wake.

Aidha alisema kuwa kwasasa mtoto huyo yupo chini ya uangalizi wa
ofisi za ustawi wa jamii jijini Arusha,ambapo anachunguzwa kiwapo
atakuwa  ameathirika na magonjwa ya zinaa ama la.

Alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mtoto huyo ameathiriwa kwa
kupata ujauzito wa miezi mitatu ambapo kulingana na umri wake ni
vigumu kuhimili maisha ya kuitwa Mama.

Baba wa mtoto huyo alipoulizwa alikiri kumwoza mtoto wake kwa mahari
ya ngómbe watatu tofauti na idadi  inayotajwa na mkwewe Ngisha.

Uchunguzi wa awali kutoka ndani ya jeshi la polisi unaonyesha kuwa
Ngisha alimchukuwa mtoto huyo tangu mwaka 2010,amabpo alipohojiwa kwa
mara ya kwanza aklikataa kosa hilo hadi siku ya jana ndipo alipokiri
kutenda kosa hilo.

Sabasi alisema kuwa kufuatia tukio hilo ababa mzazi anashikiliwa na
kumuunganisha na Baba mkwe wake,na kwamba wote wawili watafikishwa
mahakani kujibu tuhuma zianzowakabili baada ya jeshi la polisi mkoani
hapa kukamilisha uchunguzi wake kuhusiana na tukio

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia