SEREKALI YATAKIWA KUPELEKA MSWADA WA HABARI BUNGENI
KAMATI ya kudumu ya bunge maendeleo ya jamiii imeitaka serikali
kuharakisha muswada wa habari mapema ili uweze kuletwa bungeni na kujadiliwa kwa lengo la kutatua changamoto
mbalimbali ambazo zinaikumba sekta ya habari nchini.
Mwenyekiti wa kamati hiyo,Juma Nkamia alitoa tamko hilo kwa
niaba ya kamati nzima juzi mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea kituo cha
radio cha radio 5 fm kilichopo Njiro nje kidogo la jiji la Arusha.
Akizungumza mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo,Nkamia
alisema kwamba ni muda sasa serikali inatakiwa kuharakisha kuuleta muswada huo
bung ili uweze kujadiliwa na kupitishwa kwa
lengo la kuokoa sekta ya habari nchini.
“Nadhani sasa ni muda wa serikali kuharakisha mapema waulete
huu muswada wa habari ili wabunge tuweze kuujadila na kuupitisha kuokoa hii
sekta ya habari nchini”alisema Nkamia
Alisema kwamba sekta ya habari nchini imekuwa ikikabiliwa na
chanagamoto lukuki kama tatizo la waandishi kutokuwa na weledi na maadili mema hivyo muswada huo
utasaidia kuwabana waandishi hao ambao wamebatizwa jina la “makanjanja”.
Hatahivyo,aliutaka uonmgozi wa radio hiyo kujikita
kuhakikisha kwamba wanaandaa vipindi vingi vya vijijini kwa lengo la kuwapa
sauti watu wa maeneo hayo hususani wanawake na wakulima.
Awali akitoa risala yake mbele ya kamati hiyo,mkurugenzi wa
radio hiyo,Robert Francis alisema kwamba wamekuwa wakikabiliwa na changamoto
mbalimbali hususani katika maeneo ya utendaji kazi kama suala la mfumo wa
digitali.
Alisema kwamba ni muda wa kamati hiyo kuzishauri halmashauri
mbalimbali nchini kuzipatia matangazo radio zilizopo ndani ya halmashauri hizo kwa
lengo la kuongeza kipato na kuzifanya
radio hizo ziweze kujiendesha.
Alisema kwamba mikakati ya kituo chao ni kufungua chuo cha
uandishi wa habari kitakachosaidia kuwanoa waandishi mbalimbali waliopo ndani na nje kituo
hicho sanjari na kufungua kituo cha
luninga kitakachokuwa cha kwanza kurusha matangazo yake mkoani Arusha.
0 Comments:
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia