PUMZIKA SALAMA ASKOFU BALINA
Kanisa
katoliki tanzania limepata pigo kwa kifo cha Mhashamu askofu Aloysius
Balina (pichani), Askofu wa Shinyanga, kilichotokea katika hospitali ya
Bugando jijini Mwanza tarehe 6 Novemba, 2012 saa tano asubuhi. Alikuwa
na saratani.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika Shinyanga Jumamosi tarehe 10 Novemba, 2012.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika Shinyanga Jumamosi tarehe 10 Novemba, 2012.
Mhashamu
askofu Aloysius Balina, alizaliwa Juni 21,1945, Ntuzu, Bariadi mkoani
Shinyanga, Upadre mwaka 1971 na alikuwa askofu mwanzilishi wa jimbno
la Geita mwaka 1985, na baadaye akateuliwa kuwa askofu wa Shinyanga
mwaka 1997.
Kwa
zaidi ya miaka 20 amesimamia shughuli za kanisa Katoliki katika idara
ya afya, akiwa vile vile mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya rufaa ya
Bugando. Yeye ndiye mwanzilishi wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Bugando.
Marehemu alizaliwa
Juni 21,1945, Ntuzu, Bariadi mkoani Shinyanga, Upadre mwaka 1971 na
alikuwa Askofu mwanzilishi wa jimbo la Geita mwaka 1985, na baadaye
akateuliwa kuwa askofu wa Shinyanga mwaka 1997.
Kwa
zaidi ya miaka 20 amesimamia shughuli za kanisa Katoliki katika idara
ya afya, akiwa vile vile mwenyekiti wa bodi ya hospitali ya rufaa ya
Bugando. Yeye ndiye mwanzilishi wa Chuo Kikuu cha Tiba cha Bugando.
Mhashamu
askofu Aloysius Balina enzi za uhai wake akiwa na Rais Jakaya Kikwete
katika moja ya shughuli za Hopsitali ya Bugando, Mwanza
Mhashamu askofu Aloysius Balina enzi za uhai akihutubia
Mhashamu askofu Aloysius Balina akisalimiana na Laurean Kardinal Rugambwa enzi za uhai wao, na sasa wote wametangulia mbele za haki
.
.
BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE