Kufuatia Mvua Kubwa Zilizonyesha Jana Mkoani Njombe na Kusababisha
Zaidi ya Wakazi Mia Moja Kukosa Makazi Baada ya Nyumba Zao
Kuezuliwa,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe Bw George Mkindo
Amesema Kwa Sasa Wanafikiria Kuwa na Mfuko wa Maafa Utakaosaidia
Wananchi Pindi Majanga Kama Hayo Yanapojitokeza.
Akizungumza Bw Mkindo Amesema Tayari Ofisi Yake Imeshafanya
Mawasiliano na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kwa Ajili ya
Kuangalia Jinsi ya Kuwasaidia Watu Waliokumbwa na Maafa Hayo.
Aidha Pamoja na Kuezua Nyumba Hizo Pia Mvua Hiyo Ilisababisha Baadhi
ya Kuta za Nyumba Hizo Kuanguka na Kusababisha Majeruhi Kwa Baadhi ya
Wananchi Waliokuwemo Kwenye Nyumba Hizo Wakati Mvua Hiyo Ikinyesha
Wakizungumza Baadhi ya Wananchi Hao Wamesema Kufuatia Hali Hiyo
Wamejikuta Wakikosa Makazi na Hivyo Kulazimika Kujihifadhi Kwa Ndugu
na Majirani na Hivyo Kuiomba Serikali Kuwapatia Msaada wa Haraka Ili
Kuepukana na Athari Nyingine Zinazoweza Kujitokeza
Kwa upande wao viongozi wa mitaa ya kibena Otmary Mbangala,Weston
Lutumo na Bi Mary Mng'ong'o mwenyekiti wa mtaa wa kihesa Wamesema
Jitihada za Pamoja Zimekuwa Zikiendelea Ili Kuwasaidia Watu Hao
Waliokumbwa na Janga Hilo
Nyumba zilizoezuliwa paa zake ni pamoja na za Mitaa wa kibena kati
na,hospitali nyumba 100 na mtaa wa mpeto 21 na nyumba 27 za kutoka
mtaa wa kihesa kata ya Njombe mjini na mitaa ya kata ya yakobi na
mjimwema zikikumbwa kwenye mafuriko hayo
habari hii imeandikwa na mdau wa libeneke kutoka mkoani Njombe Michael Ngilangwa
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia