BREAKING NEWS

Wednesday, November 14, 2012

HALMASHAURI KUU YA CCM YACHAGUA WAJUMBE WA SEKRETARIETI YA HALMASHAURI KUU YA TAIF

 


 Abdulrahman Kinana-Katibu Mkuu wa CCM, Taifa
 Mwigulu Nchemba-Naibu Katibu Mkuu (Bara)
 Vuai Ali Vuai-Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
 Nape Nnauye-Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi
 Asha-Rose Migiro- Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
 Zakia Meghji-Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha
Muhamed Seif Khatib, Katibu wa NEC, Oganaizesheni



Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (NEC) kimekutana katika Ukumbi wa mikutano wa Makao Makuu ya chama, maarufu kama Whitehouse mjini Dodoma,leo tarehe 14th Nov 2012.  

    Kikao hicho kitajadili juu ya kuunda na kupitisha majina yaliyopendekezwa  na Mwenyekiti wa Chama Mapinduzi Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,  ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama ya Taifa (CC) pamoja na uundaji wa sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Mwenyekiti wa Chama kwa mujibu wa Kanuni na Katiba ya Chama Cha Mapinduzi, anayo fursa ya kuteua wajumbe kumi(10) wa Halmashauri kuu ya Taifa, ambapo  Mwenyekiti aliwateua wajumbe wanne(4) na akabakiza nafasi nyingine sita (6) miongoni mwa wajumbe hao ni Mhe. Asha-rose Migiro, Mhe. Zakhia Meghji, Mhe. Nape nnauye na  Mhe. Abdulrahaman Kinana .
     Baada ya uteuzi huo Mwenyekiti pia alipendekeza majina ya Wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, ambapo alipendekeza majina yafuatayo;
  1. Nafasi ya Katibu Mkuu, alimpendekeza Mhe. Abdulrahaman kinana.
  2. Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar,  Mhe. Vuai Ali Vuai.
  3. Nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara, Mhe. Lameck Madelu Nchemba.
  4. Katibu wa Oganaizesheni ni Ndugu Mohamed Seif Khatibu.
  5. Katibu wa Siasa na Mahusiano ya Kimataifa, Asha-rose Migiro.
  6. Katibu wa Uchumi na Fedha, Zakhia A. Meghji.
    Baada ya mapendekezo hayo, Halmashauri Kuu ya Taifa ilipitisha majina hayo na kuyakubali kuwa hao waliopendekezwa ndio hasa wanaofaa kuwa wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa.

     Pia, Mwenyekiti akawashukuru wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa waliopita na pia kuwataka wajumbe wapya kuchapa kazi, na kuwataka kujenga mustakabali wa Chama, Uimara na Umadhubuti kwa kufanya kazi kwa kushirikiana na kusaidiana.



Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates