Waziri
wa maliasili za Utalii Balozi Khamis Kagasheki akihojiwa na kituo cha
Televisheni ya Taifa TBC mara baada ya kutembelea mabanda ya makampuni
ya Tanzania yanayoshiriki katika maonyesho ya Utalii ya World Travel
Market yanayoandaliwa na kufanyika katika eneo la Excell jijini London
nchini Uingereza, yakishirikisha makampuni mbalimbali ya utalii kutoka
pande zote za dunia, Mwaka huu Tanzania inawakilishwa na makampuni zaidi
ya 55 yakiwa chini ya Bodi ya Utalii nchini Tanzania (TTB).
Waziri
Balozi Kagasheki amesifushiriki wa makampuni ya Tanzania katika
maonyesho hayo lakini amesisitiza kwamba makampuni hayo yaongeze juhudi
za kutangaza utalii wa Tanzania mpaka kufikisha lengo la idadi ya
watalii milioni moja kila mwaka, ameongeza kwamba kuna haja ya kuongeza
vitanda zaidi nchini Tanzania ili kuongeza idadi ya watalii
watakaotembelea katika mbuga zetu na kufanya utalii kuka zaidi,
Maonyesho hayo yatazinduliwa rasmi kesho.
Waziri
aliasili na Utalii wa Balozi Khamis Kagasheki akisalimiana na Issa
Ahmed Othman Mshauri wa Rais masuala ya Utalii Zanzibar wakati
alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho ya utalii ya (WTM)
jijini London leo nchini Uingereza
Waziri
Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Leila Ansel Mkuu wa mauzo na
masoko kampuni ya Tanzania Zara Adventures wakati alipotembelea katika
banda hilo leo kwenye maonyesho ya utalii ya WTM nchini Uingereza.
Yvone
Baldwin Afisa mauzo wa kampuni ya ndege ya Precision Air akimkabidhi
zawadi Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mh. Peter Kallaghe mara baada
ya kutembelea banda hilo leo akiongozana na Waziri wa Maliasili Balozi
Khamis Kagasheki.
Waziri
wa Maliasili Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Rashid Adam Meneja
Masoko wa Tanzania Zara Adventures wakati alipotembelea maonyesho ya
Utalii ya WTM katika banda la Tanzania leo jijini London, wa pili kutoka
kushoto ni Mh. Peter Kallaghe Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na
katikati ni mama Balozi.
Waziri
Balozi Khamis Kagasheki akizungumza na Laura Meneja wa Maendeleo ya
Biashara kampuni ya Laitolya Tours & Safari Ltd kushoto wakati
alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonyesho ya WTM leo, kulia
ni Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi.
Mkurugenzi
wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi akiwahudumia
watu mbalimbali waliotembelea katika banda la Tanzania leo katika
maonyesho ya Utalii ya WTM jijini London Uingereza
Meneja
Masoko wa Bodi ya Utalii ya Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena akiwa katika
picha ya pamoja na wakurugenzi wa African Environments Richard Beatty
na Janice Beatty katika maonyesho hayo.
Leila
Ansel Mkuu wa mauzo na masoko kampuni ya Tanzania Zara Adventures
akizungumza na mmoja wa wageni waliotembelea katika banda la kampuni
hiyo katikati ni Rashid Adam Meneja Masoko wa Tanzania Zara Adventures.
Mh.
Peter Kallaghe Balozi wa Tanzania nchini Uingereza akizungumza na mdau
Juma Mabakila wakati akitembelea banda la Tanzania kwenye maonyesho ya
WTM
Meneja
Masoko wa Bodi ya Utalii ya Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena
akiwasikiliza wageni mbalimbali waliofika katika banda la Tanzania
katika maonyesho hayo leo.
Balozi Khamis Kagasheki Waziri wa Maliasili Utalii wa
pili kutoka kulia akizungumza na Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii
Tanzania TTB Devotha Mdachi mara baada ya kutembelea Banda la Tanzania
katika maonyesho ya Utalii ya WTM nchini Uingereza , kulia ni Mh. Peter
Kallaghe Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na katikati ni Mama Balozi.
Mmoja
wa washiriki kutoka kampuni ya Africa Adventure akihojiwa na kituo cha
televisheni cha TBC katika maonyesho ya Utalii ya WTM yanayofanyika
jijini London nchini Uingereza.