wananchi wakiwa wanashuhudia haiece iyo ambayo inafanya safari zake Arusha mjini _kikatiti ikiwa ndani ya mto themi uliopo karibu na bar ya manchester jijini hapa leo mchana ilivyodumbukia
muonekano wa hiece hiyo kwa sasa |
Wananchi wakiwa wanashughudia gari hiyo jinsi ilivyoharibika mara baada ya majeruhi kukimbizwa hospitali ya mkoa ya mounti meru jijini Arusha
Leo majira ya saa nane mchana maeneo ya manchester njia katika barabara ya Arusha -Moshi kwenye daraja la mto Themi kumetokea ajali mbaya ya gari aina ya Hiece ambayo namba zake hatujaweza kuzipata na watu baadhi ya watu waliokuwa kwenye ajali hiyo wamejeruliwa vibaya sana.
Gari hiyo ambayo ilikuwa inatokea usa kuja jijini arusha ilidumbukia katika daraja hilo huku mpaka libeneke la kaskazini linaondoka eneo la tukio bado akijabainika haswa chanzo cha ajali hiyo kwani kuna baadhi ya watu walikuwa wanasema ajali hiyo imesababishwa na mwendo kasi huku wengine wakisema kuwa gari hiyo ilikosa breki hali iliyosababisha minongono mingi kati ya watu waliotokea kushughudia ajali hiyo.
Kwa taarifa za pale hamna ata mtu mmoja ambaye alifariki dunia lakini libeneke la kaskazini blog linaendelea kufuatilia na tutawajuza taarifa zaidi
kikubwa tunachoshauri madereva wafuate sheria za barabarani ili kuepusha ajali za mara kwa mara