KATIBU mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo
CHADEMA Dkt,Willbrod Slaa amemtaka rais
Jakaya Kikwete ambaye ni
mwenyekiti wa ccm Taifa, kutotumia muda mwingi kuvishambulia vyama vya siasa
ikiwemo chadema, badala yake atumie muda huo kuzungumza ni namna ya kutatua
kero za wananchi ili kupunguza ukali na ugumu wa maisha unao wakabili kwa sasa.
Dkt Slaa aliyesema hayo
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika mahakama kuu ya kanda ya
Arusha kuhusiana hoja mbalimbali zilizozungumzwa katika mkutano wa CCM
uliofanyika jangwani Juzi pamoja na mstakabali ya taifa kuhusiana na maswala
mbalimbali yanayowakabili wananchi.
Akijibu shutuma mbalimbali
zilizotolewa katika mkutano wa kuwapokea viongozi mbalimbali wa ccm
waliochaguliwa mjini Dodoma alisema kuwa,
katika mkutano huo viongozi wengi wa ccm akiwemo rais kikwete alitumia muda
mwingi kuelekeza nguvu zao jinsi ya kukabiliana na vyama pinzani katika uchaguzi
mkuu ujao 2015 .
Alisema ccm imeelekeza
nguvu zake kujifua ili kukikabili chadema katika uchaguzi ujao mwaka 2015 na
sio kuwaeleza wananchi nini watawafanyia ili kuwaondoa katika janga la umaskini
huku akiwatuhumu kuchukua sera mbalimbali
zilizoanzishwa na ikiwemo ya kusomesha wanafunzi bure kwa shule za shekondari
na msingi.
“kibaya zaidi nashindwa
kuelewa kuwa Kikwete ajui kuwa anadanganywa au la mimi juzi wakati natokea dare s salam
nilikutana na misururu mirefu ya mabasi ambayo yalikuwa yamepakia makundi ya
wanachama wa ccm waliokuwa wakielekea dar sasa mimi nashindwa kuelewa kuwa kuwa
kikwete anatambua haya au la na kama hatambui ajue anadanganywa na ni ufisadi anafanyiwa na usifasadi sio lazima
uwe wa fedha tu bali ata kudanganywa ni ufisadi tosha”alisema Dr,slaa
Adha katika hatua nyingine
alisema kuwa anamshangaa sana rais kumteua katibu mkuu wa chama cha mapinduzi
Abarahaman Kinana wakati sio msafi kushika wadhifa huo kwani anakabiliwa na
kashfa mbaya ya kusafirisha pembe za ndovo (meno ya tembo) ambayo ni meno mia
563 ambayo ni sawa sawa na tembo 250 ambazo zilisafirishwa kwenda nchini china
“na kizuri zaidi kinana
mwenyewe amekiri meli ya kampuni yake ilihusika kusafirisha huku saini za wafanyakazi wake zipo lakini
tunamshanga ajakiri kuwa meno yalikuwa
yanasafirishwa na kampuni yake ni
yakwake au la au angemtaja ningefurahi kama angesema kuwa meno yale ni ya nani
na sio kukaa kimnya maana watu wake pia wamesaini zile nyaraka za kusafirisha”alisema
slaa.
Alisema kuwa anampaje mtu huyu
madaraka ya kusimamia serekali iliyojaa njaa na ufisadi wakati anamjua anamaovu
huku akisema kuwa huu ni uzalilishaji mkubwa katika serekali kwa ujumla na
chama husika.
Dr,Slaa alisema kuwa katika
safun hiyo mpya hamna jambo jipya analoliona
na wala hao nitu kipya ambacho safu hii uliyochaguliwa itaifanya kwani
chama cha ccm ni sawa na glasi uiliyojaa maji na pia alisema kuwa chama hicho
kimeishiwa ubunifu
Aidha aliwatuhumu chama
tawala kwa kwakitendo cha kuchukuwa sera zinazotungwa na chadema akitolea mfano
sera ya elimu bure ambayo waliibua katika kampeni za uchaguzi za mwaka 2010
huku akisema kuwa wao hawachukii sera zao kuchukuliwa na chama tawala bali
wanataka pale zinapochukuliwa zifanyiwe kazi na wananchi wanufaike.
Alibainisha kuwa kazi ya
chama cha upinzani ni kuibua changamoto mbalimbali na mapungufu ya utendaji wa
chama tawala hivyo wao kama chadema wataendelea kuibua na kuyasema hadharani
mapungufu ya serikali hadi pale itakapo tekeleza.