BREAKING NEWS

Saturday, November 10, 2012

RIPOTI YA UNESCO YAONYESHA KUWA ELIMU BADO NI KIKWAZO KIKUBWA KWA USTAWI WA VIJANA TANZANIA NA AFRIKA.


Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Dkt. Alberic Kacou akizungumza wakati wa uzinduzi wa ‘Education for All Global Report’ ya mwaka 2012 inayoandaliwa na UNESCO kila mwaka, ambapo pamoja mambo mengi aliyoyazungumzia pia amesema tukiwa tumebakiwa na si zaidi ya miaka mitatu kufikia mwaka 2015, michakato ya kutimiza Malengo ya Maendeleo ya Millenia (MDGs) na Malengo ya ‘Elimu Kwa Wote’ (EFA) lazima irekebishwe.
Ameongeza kuwa japo Tanzania inakaribia kutimiza lengo namba 2 la MDGs la ‘Elimu ya Msingi kwa Wote na lengo la Tatu la Usawa wa Kijinsia lakini bado ziko changamoto, akitolea mfano katika elimu na kusema msisitizo umeelekezwa katika kuongezwa kwa idadi ya watoto wanaojiunga shule lakini kimsingi kinachotakiwa ni kuweka mkazo kwenye kiwango cha elimu kinachotolewa.
Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen akiwasilisha matokeo ya ripoti ya 10 ya ya mwaka 2012 ya ‘Education for All Global leo jijini Dar es Salaam inayoitwa “Putting Education to Work” na kufafanua kuwa takriban vijana milioni 2 nchini Tanzania hawajamaliza elimu ya msingi na hawana maarifa ya kuwapatia kazi itakayowapatia kipato cha kujikimu kimaisha.
Amesema matokeo ya ripoti hiyo yanaonyesha kuwa juhudi za haraka zinahitajika ili kuwekeza katika kuwapatia vijana elimu haswa wenye miaka kati ya 15 hadi 24 Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.
Mwenyekiti wa Taifa Chama cha Vijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA) Bw. Lwidiko Edward Mhamilawa akizungumza katika uzinduzi huo na kuitaka Serikali kuangalia upya Sera ya Elimu kwa kuwa haimwezeshi Mhitimu kuwa na uwezo wa kufanya kazi itakayomwezesha kuendesha maisha yake na hivyo kuwa moja ya changamoto kubwa inayoongeza idadi ya vijana wasiona ajira mtaani.
Kamishna wa Elimu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Eustella Bhalalusesa wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo ambapo amesema Tanzania itaendelea kufanya kazi bega kwa bega na mashirika ya Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha Sera za Elimu zinaboreshwa ili kuinua kiwango cha Elimu na kumjenga kijana kuwa na stadi za kukabiliana na maisha hata kama hakufaulu darasani.
Mwakilishi wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania (ILO) Bw. Alexio Musindo akisisitiza ili kuboresha elimu walimu wanahitaji kupewa mafunzo bora, kupatiwa vifaa vya kufundishia na mtaala wa Elimu kutoka ngazi ya Taifa mpaka ngazi za chini unahitaji kufuatiliwa na kusimamiwa.
Moderator wakati wa kuchangia maoni Juu ya Ripoti hiyo Profesa Idrissa Mshoro akitoa tathmini yake kuhusiana na matokeo ya "Education For All Global Monitoring Report" kabla ya kutoa nafasi kwa jopo la wataalam waliohudhuria kuendelea na uchambuzi wao.
Jopo la Wadau wa Kimataifa wa Elimu wakitathmini Ripoti ya UNESCO ya Mwaka 2012. Kutoka kushoto ni Moderator Profesa Idrissa Mshoro, Deputy Head of Mission, Head of Development Cooperation Division Ubalozi wa Sweden B. Maria Van Berlekom, TVET Section Makao Makuu ya UNESCO Paris Bw. Borhene Chakroun, Senior Technical Advisor, Education for Employment Bw. Peter Loan na Mjumbe wa Bodi ya Chama cha Waajiri Tanzania Bw. Kabeho Solo.
Meneja Mipango wa Ubalozi wa Shirika la Maendeleo la Itali katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi hiyo katika Ubalozi wa Italia nchini Bw. Daniele Cristian Passalacqua akichangia maoni juu wakati wa uzinduzi wa ripoti hiyo. Kulia ni Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Bi. Vibeke Jensen.
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou na Mwakilishi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) nchini Tanzania Bw. Alexio Musindo.
Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya wadau mbalimbali kutoka Mashirika ya Maendeleo, Mashirika ya Kijamii na Sekta Binafsi.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates