KAMPUNI ya Travel port
(Galileo) yenye makao yake makuu jijini Dar es salamu imezindua teknolojia mpya jijini Arusha ya kuuza tiketi za ndege kwa kupitia simu za mikononi , huduma
ambayo itawawezesha wateja na mawakala kufanya kazi kwa haraka na ufanisi zaidi.
Akizindua huduma hiyo kwa
mawakala zaidi 30 wa mashirika ya ndege jijini Arusha, Afisa mwandamizi kitengo
cha huduma kwa wateja kutoka kampuni hiyo, bw Robert Mahina alisema teknolojia hiyo ni mpya na utarahisisha upatikanaji wa teketi
za ndege na ratiba za mashirika ya ndege ndani na nje ya nchi.
Bw Mahina alisema kuwa, huduma
hiyo ambayo ni ya pili kuzinduliwa mkoani Arusha baada ya kuzinduliwa jiji Dar
es Salaamu, itawawezesha wateja wake
kuweza kupata huduma kwa haraka popote
walipo ikiwemo kujua ratiba za makambuni ya ndege kwa kutumia simu za mkononi
ambazo zitakuwa zimeunganishwa moja kwa moja na kampuni hiyo.
Aliongeza kuwa, teknolojia
hiyo mpya ambayo imekuwa ikitumiwa zaidi na mashirika ya ndege nje ya nchi
itawawezesha kurahisisha utendaji kazi na kutambua huduma zinazotolewa na
mshirika mbalimbali ya ndege bila kufika kwenye ofisi za mashirika ya ndege au
kuwasiliana na wahudumu kwani tayari huduma hiyo itakuwa imeunganishwa kupitia
simu zao za mkononi.
Bw Mahina aliongeza kuwa,
mchakato huo ambao tayari umeanza mwezi huu una manufaa makubwa sana kwa
watumiaji kwani inawawezesha kupata maelezo mbalimbali wanayohitaji kwa wakati
ikiwa ni pamoja na kuwapatia huduma wateja wake popote pale walipo bila kufika ofisini.
Alifafanua zaidi kuwa, kabla
ya kuzinduliwa kwa teknolojia hiyo mpya
ilikuwa ikiwalazimu mawakala na wateja kufika ofisini kufuatalia tiketi zao
hali ambayo ilikuwa ni changamoto kubwa kwani walikuwa wakitumia muda mwingi
kupata huduma hiyo tofauti na ilivyo hivi sasa.
‘Unajua teknolojia hii mpya
ndio inatumiwa na wenzetu nje ya nje ya teknolojia, hivyo tumeona ni nzuri sana
na hivyo tukaamua kuileta kwetu ili iweze kutuletea manufaa ikiwemo kurahisisha
huduma inayotolewa kutoka kwa wakala kwenda kwa mteja na mteja naye kuweza kunufaika
kwa kuwasilina na wakala kupitia simu yake ya mkononi’alisema bw Mahina.
Alisema kuwa, teknolojia
hiyo imeshazinduliwa jijini Dar es Salaamu ambapo wanatajia kuizindua Zanzibar
na Mwanza ambapo huduma hiyo inatarajiwa kuwafikia wateja wote nchini wanaotumia
simu zenye uwezo wa kupokea huduma ya
intaneti “Smart Phone’ .
Alitoa wito kwa wadau
mbalimbali wa usafiri wa ndege kutumia teknolojia hiyo kwani ina manufaa
makubwa sana na inaokoa muda, haikabiliwi na changamoto yoyote ikiwemo kusumbua
kwa mtandao kama ilivyo kwenye computer .
Kwa upande wa mawakala wa mashirika
ya ndege mkoani hapa walioshiriki
mafunzo hayo wameonyesha kufurahia huduma hiyo kwani itawasogeza karibu na
wateja wao na kuwapunguzia kazi ya kufanya mawasiliano ya mara kwa mara na wateja
hali ambayo ilikuwa inawawia vigumu kuitoa huduma hiyo kwa wakati .