MWENYEKITI wa kijiji
cha Losirwa kata ya Esilalei wilayani Monduli bwana George Arpakwa
ametuhumiwa na wananchi wake kujihusisha na ufisadi wa uuzaji wa ardhi kiholela
ya kijiji swala ambalo linakwamisha shughuli za kifugaji kijiji hapo.
Wananchi wa kijiji
hicho wakizungumza kwa masikitiko makubwa katika mkutano wa hadhara kijiji hapo
wamedai kuwa wamechoshwa na uongozi wa mwenyekiti huo kushindwa kuonyesha
uwadilifu wake kwa jamiii badala yake kuuza ardhi ya kijiji kinyume na sheria.
Mwenyekiti wa kijiji
hicho ambae anatuhumiwa kujihusisha na kuuza ardhi ya kijiji baada ya kubaini
kuwepo kwa waandishi wa habari eneo hilo alichukua jukumu la kuvunja
mkutano na kuleta vujo kwa baadhi ya viongozi wa kimila akidai kua
waandishi wa habari hawaruhusiwi kuhudhuria mkutano huo huko akitokomea pasipo
julikana.
Aidha Romeni ole Meiya
akiwa mmoja wa kijiji hicho alisema kua alishangazwa sana kuona baadhi ya
maeneo ya malisho ya mifugo na mapito ya mifugo sambamba na mabwawa kuwekewa
uzio kuashiria kua mifugo hairuhusiwi kuingia eneo hilo licha ya maeneo hayo
yakiwa yametengwa kwaajili ya mifugo.
Alisema hawana imani
tena na mwenyekiti huyo wa kijiji ambae sasa ameonyesha udhaifu
wake katika utendaji wake wa kazi hivyo wanamtaka achie ngazi na kwasasa
hawamtambui kama yeye nikiongozi wa jamii hiyo ya kifugaji kwa kujihusisha na
kuuza ardhi ya wafugaji kinuyme na sheria za kijiji husika.
Nae Kiteho
Richard alisema kunaashiria kijiji hicho kuwepo kwa ufisadi mkubwa
wa ardhi huku akihoji kwanini mwenyekiti alipobaini kuwepo kwa waandishi
wa habari eneo hilo kutokomea pasipojulikana huku akijua waandishi ni
watu wa amani siku zote.
"Kama mwenyekiti
hahusiki na kuuza maeneo ya wananchi kwanini amekimbia mkutano hii inaonyesha
kua anahusika kwa asilimia kubwa ndio mana alipowaona waandishi wa habari
akakimbia akijua siri inafichuka" Alisema Richard"
Wananchi hao
waliandamana hadi ofisi ya mwenyekiti huo nakuchukua jukumu kali lakutaka
kuifunga ofisi hiyo wakiamini kua ninjia moja wapo ya kupata suluhisho la Ardhi
yao kumilikiwa na wenye pesa wachache huku wakiomba serikali kushughulikia
tatizo hilo likiwa bado halijaleta hadhari kubwa kwa jamii.
Kwa upande wake mkuu
wa wilaya ya Monduli bwana Jowika Kasunga akizungumza kwa njia ya simu amekiri
kupokea taarifa hizo za malalamiko ya wananchi nakuahidi kuwa anazifanyia kazi
ilikubaini ukweli wa jambo hilo.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia