Kikosi cha maswala ya ulinzi katika jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika(SADC) kimesema kuwa akitaendelea kufungia macha mapigano yanayoendelea katika mji wa Goma uliopo mashariki mwa nchini kongo .
Hayo yalibainishwa mkuu kikosi cha secretariti ya ulinzi na mipango katika nchi za SADC kanali Gerson Sangiza wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na namna gani kikosi cha ulinzi kinasaidia mapigano ya nchini kongo.
Alisema kuwa katika kipinchi cha nyuma walikuwa bado ya wapo katika mazungumzo ya kujadili ni jinsi gani wanaweza kuisaidia nchi hii kongo kuondokana na mapigano ambayo yameikumba nchi hiyo kwa muda mrefu .
Alisema kuwa kwakua majeshi ya nchi za sadc yameundwa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi pamoja na kuwalinda hivyo wanajipanga vilivyo kwa ajili kupeleka kikosi nchini kongo ya ili kuwasiadia wananchi wa nchini humo ambao wameteseka kwa muda mrefu.
Pia alifafanua kuwa majeshi ya nchi za sadc yameendelea kushirikiana kwa kipindi cha mda mrefu kwa katika mambo mbalimbali ikiwemo viongozi wa nchi zetu kushirikiana kwa kupeana ziara zakikazi,mafunzo ya kijeshi yakitolewa katika nchi yetu ambapo alifafanua kuwa chuo cha kijeshi cha TMA kimekuwa kikichukuwa wanafunzi kutoka nje ya nchi hususa ni nchi za sadc nawaleta kuwapa elimu hapa nchini kwetu.
"pia tumekuwa tukitumia viongozi wetu ambapo wamekuwa wanabadilishana ziara ambapo lengo kuu la ziara hizo ni kubadilishana uzoefu pamoja na kujenga mahusiano"alisema Sangiza
Alisema kuwa kazi nyingine ya majeshi haya ya sadc ni pamoja na kuwalinda wananchi wa nchi hizi 15 na kuhakikisha kwamba kanda yetu hii haitaingia tena katika machafuko
Aliongeza kuwa majeshi haya yatasaidia pia wanachi wasiweze kupata matatizo na pia kuhakikisha machafuko hayawezi kutokea katika nchi hizi ili hali ya utulivu na amani iendelee kuwepo ili maendeleo yawezekuwepo.