RAIS AZINDUA MKAKATI WA MASWALA YA SIASA ,ULINZI PAMOJA NA USALAMA

 VIONGOZI WA SADC wakiongozwa na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya mrisho kikwete katika picha pamoja
 Muheshimiwa rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania akifafanua jambo katika mkutano wa SADC uliofanyika leo katika hotel ya ngorudoto
kikundi cha ngoma kikitumbuiza nje ya hotel ya ngorodoto
Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr.Jakaya Mrisho kikwete leo amezindua rasmi mkakati wa pili utakao shirikisha nchi za SADC utakao  shughulikia maswala  ya Siasa,Ulinzi pamoja na usalama  .

Akizindua mkakati huo wa nchi za SADC leo katika hotel ya Ngurudoto iliopo nje kidogo ya jiji la Arusha alisema kuwa huu ni mkakati wa pili kuzinduliwa kwani mnamo mwaka 2004 mkakati wa kwanza wa  ushughulikiao maswala ya siasa ,ulinzi na usalama katika nchi za SADC ulizinduliwa ila ulikuwa haujitoshelezi kutokana na  kuwepo kwa mapungufu mengi .

Aidha alibainisha kuwa mara baada ya nchi hizo kubaini kuwa mkakati huo unamapungufu waliamua kufanya tasmini upya  kuanzia mwaka 2009 na nchi zote zilitoa maoni upya na kurekebisha sehemu ambazo zina mapungufu ambapo alibainisha kuwa katika mkakati uliopita kuna mambo mengi yalikuwa hayajaingizwa ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na mtikisiko wa uchumi hivyo kurekebisha  na mara baad aya kukamilika waliamu kuupitisha upya na jana (leo) ndo wamezindua rasmi na umeanza kufanya kazi rasmi.


Alisema kuwa shughuli moja wapo ambayo mkakati huu wa SIPO utaanza nao ni pamoja na kutatua matatizo yaliyopo DRC kongo ambapo alisema kuwa nchi hii inakabiliwa na mapigano makali yanayowahusisha wahasi wa kikundi cha M23 ambapo inapigana kwa mda mrefu na serekali ya kongo hivyo wao kama umoja wa nchi za SADC  wameshauriana na viongozi kuona ni namna gani wanaweza kuzuia mapigano hayo yasiendelee na si hivyo tu bali wanaangalia ni jinsi gani wataweza kuwasaidia wananchi wanaoteseka nchini kongo.

Kikwete alisema kuwa  katika kutatua tatizo hili nchi za SADC kwa kushirikiana na nchi za jumuiya ya maziwa makuu walishakaa kuongelea tatizo hili na walishakaa nchini Adis ababa kuongelea tatizo hili pamoja na kampala hii yote ni kutafuta jawabu la kutatua mgogoro  wa nchini kongo katika eneo la Gomu .

Adha  kwa upande wa mgogoro wa nchi ya Malawi na Tanzania kama utaweza kutatuliwa na SADC alisema kuwa  mgogoro huo bado haujafikia katika kiwango cha dunia kwani  mapaka sasa bado nchi yetu inamazungumzo na malawi na iwapo muhafaka hautapatikana basi watapeleka huko  ila ni mapema sana kwa sasa kupeleka  swala hilo wakati mazungumzo bado yanaendelea.

"hili swala la malawi bado alijaletwa katika nchi za sadc kwani bado tupo katika mazungumzo  na naamini kabisa tutaelewana ila ikishindikana basi tutaleta huku ili muafaka upatikane maana kazi ya mkakati huu au chombo hichi cha tulichokizundua leo ndo kinashughulikia maswala hayo "alisem kikwete

Aimalizia kwa kusema kuwa anaimani kuwa mkakati huu  uliozinduliwa leo utaweza kusaidia nchi hizi zilizopo katika jangwa la sahara kwa kiasi kikubwa katika kupunguza mambo mbalimbali kama uhalifu.

Katibu mkuu wa SADC   Tomaz Augusto Salomao alisema kuwa mkakati huo utaweza kusaidi  nchi hizi zilizopo katika jagwa la sahara katika mambo mengi yakiwemo ya kiuchumi ,utamaduni,siasa pamoja na ulinzi

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post