wachezaji wa timu ya mpira wa pete wa timu ya bunge wa jamuhuri ya
muungano wa tanzania waliovaa nyeusi wakicheza mpira na timu ya chuo cha
arusha tekniko katika uwanja wa sheikh amri abeid hivi leo ambapo timu
ya bunge iliibuka mshindi mara baada ya kuifunga timu hiyo 24 -13
Lucy kiwelu akiwa anamkaba mpinzani wake katika mashindano hayo ya bonanza la jumuiya ya Afrika mashariki linaloendelea kufanyika jijini Arusha
picha juu na chini ni Washabiki wa timu ya wabunge wakiwa wanaangalia mpira safi
Mama wa CCM viola wa pili kutoka kushoto alikuwepo pia akiangalia mechi hiyo
Timu ya bunge la jumuiya ya afrika mashariki ikipewa mawaidha na kocha wake Rashid wakati wa mapunziko ya kipindi cha kwanza
Timu ya bunge la jumuiya ya afrika mashariki iliyovaaa blue ikicheza na timu ya Taswa FC ya jijini Arusha ambapo walitoka kwa twaswa kufungwa bao 2-1
pia katika bonanza hilo la jumuiya ya afrika mashariki kulikuwa na wajasiriamali kibao kutoka nchi mmbalimbali ambao ambao wameshiriki katika tamasha hilo
Timu ya Bunge
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania(Bunge sports club) imeweka kambi ya
wiki mbili Jijini Arusha kwa ajili ya mashindano kombe la Jumuiya ya Afrika Mashariki yatakayo timua vumbi
jijini Nairobi nchini Kenya.
Akizungumza na
waandishi wa habari mwenyekiti timu hiyo
ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kinondoni
Idd Azan alisema kuwa pamoja na majukum waliyonayo bado wana nafasi kubwa ya kushiriki miashindano hayo na kuhakiksha
kuwa kombe hilo linarudi Tanzania.
Azan alisema
kuwa lengo la michuano hiyo ni kushirikiana na wabunge wa nchi nyingine
zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kudumisha umoja na kuwa na mshikamano
kupitia michezo.
Aidha alieleza
kuwa lengo lingine ni kudumisha ushirikiano
wa Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na kuwapa burudani wananchi wa nchi zinazounda Jumuiya husika.
Pia alisema
kuwa timu hiyo ya wabunge ya mpira wa miguu na mpira wa pete zipo katika hali
nzuri na tayari wamesharekebiha mapungufu yaliyojitokeza katika michuano
iliyopita ili waweze kurudi na kombe hilo la Jumuiya Ya Afrika Mashariki.
‘’Timu yetu
ipo katika hali nzuri na tayari tumeshafanya marekebisho ya makosa tuiyofanya
kipindi cha nyuma hivyo watanzania watarajie ushindi kwa kuwa wachezaji wote
wapo katika hali nzuri.”alisema Azan
Hata hivyo
timu ya mpira wa pete ya wabunge imeichapa timu ya arusha technical magoli
24-13 katika mtinange uliochezwa katika dimba la Sheikh Amri Abeid Jijini
Arusha.
Katika mtnange
mwingine timu ya mpira wa pete ya ngorongoro creater imechapwa magoli 42-31 na
timu ya Mpira wa pete ya jijini Arusha.
Kesho timu
ya wabunge sports itacheza na timu ya mpira wa miguu ya waandishi wa habari
jijini hapa (taswa)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia