Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akipongezwa na aliyekuwa
Msimamizi wa Uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Makamu wenyeviti
wawili, Spika wa Bunge Anna Makinda, baada ya kumtangaza kushinda nafasi
hiyo ya Uenyekiti, katika uchaguzi uliofanyika hivi punde katika ukumbi
wa Kizota, Dodoma, ikiwa ni kuhitimisha shughuli za Mkutano Mkuu wa
Nane wa CCM. Wapili Kulia ni Makamu Mwenyekiti Mpya wa CCM (Zanzibar)
Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Dk. Moahamed Gharib Bilal
Mwenyekiti wa CCM, Taifa, Jakaya Kikwete na Makamu wake wawili Rais wa
Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein (Zanzibar) na Philip Mangula (Bara)
wakiwa meza kuu baada ya kutangazwa kushika nyandhifa zao.
Wajumbe wakiserebuka baada ya Rais Jakaya Kikwete kutangazwa kuwa mshindi wa Uenyekiti wa CCM, Taifa.
Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete akiongoza kikao baada ya kushinda tena
kiti hicho. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk. Ali
Mohamed Sheni na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Phili Mangula.PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO