Wafanyakazi wa kiwanda cha
kutengeneza vyandarua na t.shirt cha ATOZ cha Jijini Arusha wamedai kuwa uongozi
wa kiwanda hicho umemudanganya Rais Dkt Jakaya Kikwete kuwa wafanyakazi wa
kiwanda hicho wanalipwa maslahi mazuri.
Rais Kikwete wiki iliyopita
katika ziara yake Mkoani Arusha alifanikiwa kukitembelea kiwanda hicho na kituo
cha utafiti kilichopo kiwandani hapo na ujionea shughuli mbalimbali za
maendeleo zinazofanywa na wafanyakazi hao.
Wafanyakazi zaidi ya 10
wakiongea na waandishi wa habari walisema kuwa ni baadhi ya wafanyakazi wa
idara ya kutengeneza mifuko ya sembeti nay a kawaida ndio wanalipwa vizuri kwa
kiasi cha shilingi 180,000 ukiondoa makati.
Mfanyakazi huyo ambaye
aliomba kutotajwa jina lake
alisema idara zingine
hulipwa mshahara wa fedha raslimu shilingi 105,000 baada ya makato kwani kwenye
karatasi za malipo {par roll} huonyesha shilingi 130,000 tu.
Alisema mbali ya hilo mfanyakazi anayeumia kazi kama
vile kukatwa mkono na mashine na kupata ajali kazi mfanyakazi hukopeshwa fedha
na uongozi wa kiwanda ili apate matibabu na baadae hukatwa katika mshahara
wake.
‘’Sasa tumeambiwa tuimbe
nyimbo za kumsifu Rais na kuusifu uongozi wa kiwanda kwa kulipwa vizuri mbele
ya Rais wakati sio kweli huku ni kumdanganya Rais ‘’alisema
Mfanyakazi mwingine ambaye
pia aliomba asitajwe gazetini alisema uongozi wa kiwanda haulipi malipo ya kazi
ya ziada{over time},haulipi malipo ya kodi ya pango na umekuwa ukiwanyanyasa
wafanyakazi kama enzi za utawala wa makaburu
nchini Afrika ya kusini.
‘’tunawaomba nyie waandishi
wa habari andikeni ukweli juu ya kiwanda kile cha ATOZ kwani kuna mambo makubwa
sana uongozi wa
serikali unapaswa kuyajua na kuyafanyia kazi lakini mkikaa kimya mtawaangamiza mamia
ya wananchi waliopo pale’’alisema mfanyakazi huyo.
Alisema mfanyakazi
anachukuliwa majira ya saa 12 asubuhi kuingia kazini na bus la kampuni na
kurudishwa saa 1.30 usiku,mfanyakazi anafanya kazi kama
punda zaidi ya masaa 12 tofauti na kawaida ya mfanyakazi kufanya kazi masaa 8
tu.
Akizungumzia hilo Mkurugenzi Mtendaji msaidizi wa kiwanda
cha ATOZ ,Godwini Abeid alipinga na kusema kuwa madai yaliyotolewa na
wafanyakazi hao hayana ukweli hata mmoja na kueleza kuwa ni uzushi uliotungwa.
Abeid alisema mbali ya
kuajiri mamia ya wafanyakazi katika kiwanda hicho alisema hakuna mfanyakazi
anayelipwa kiwango cha mshahara wa serikali cha shilingi 80,000 kwani
wafanyakazi wote wanalipwa juu ya kiasi hicho.
Alisema suala la mfanyakazi
kukatika mkono ama kuumia akiwa kazini kiwanda ndio kinagharamia matibabu yote
na hakuna mfanyakazi aliyekatwa mshahara kwa ajili kufidia matibabu yaliyolpwa
na uongozi wa kiwanda.
‘’hapa kila kitu kipo sawa na
tunalipa vizuri misharahara na masaa ya ziada na kama
kuna wafanyakazi wamekuja kulalamika na kusema uongozi umemdanganya Rais sio
kweli bali wao ndio wamewadanganya nyie ‘’alisema
Naye Mwenyekiti wa chama cha
wafanyakazi wa viwandani{TUICO} Rehema Abdallah alisema kuwa yeye kama mtetezi
wa haki za wafanyakazi kwa kushirikiana na kamati yake wako mstari wa mbele
kuhakikisha maslahi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho wanalipwa vizuri .