Mkutano mkuu wa nchi zilizotia saini mkataba wa kuanzisha Mahakama
ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) umefunguliwa Jumatano mjini the
Hague, Uholanzi huku nchini Rwanda,wakili wa mshitakiwa wa mauaji ya
kimbari, Leon Mugesera adai kuwa mteja wake atendewa isivyo haki ndani
ya jela za nchi hiyo.
ICC
Gbagbo akataliwa dhamana kwa mara ya pili: Mahakama ya Kimataifa ya
Makosa ya Jinai (ICC) Jumatatu imemnyima dhamana kwa mara pili Rais wa
zamani wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo
na kumwamuru kubakia rumande.Uamuzi huo unafuatia pia kushindwa kwa
kiongozi huyo kuishawishi mahakama hiyo kuahirisha kusikilizwa kwa kesi
yake kutokana na sababu za kiafya.Gbagbo anashitakiwa kwa uhalifu dhidi
ya binadamu unaodaiwa kufanywa baada ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo
Desemba 2010.
Bemba ataka DRC kuwa na umoja: Kiongozi wa zamani wa waasi katika
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Makamu wa Rais wa nchi hiyo
Jean-Pierre Bemba ametoa wito kutoka katika jela anayoshikiliwa mjini
The Hague, Uholanzi kwa wafuasi wake kumaliza vita inayoendelea
Mashariki mwa nchi hiyo. Katika ujumbe wake pia, Bemba ameiomba serikali
ya nchi hiyo kumaliza vita hiyo na vitisho vya usalama katika ukanda
huo ili kulinda usalama wa raia.Amewataka raia wa nchi hiyo kuwa na
umoja na maridhiano ili kuinusuri nchi yao.
Nchi zilizounda ICC zakutana Uholanzi: Mkutano mkuu wa nchi zilizotia
saini mkataba wa kuanzisha Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai
(ICC) umefunguliwa Jumatano mjini the Hague, Uholanzi katika sherehe
ambazo pia zilihudhuriwa na Malkia Beatrix wa nchi hiyo.Akizungumza
katika sherehe hizo, Rais wa Mkutano huo,Tiina Interlman alisema ICC
haina budi kufanya mabadiliko ya msingi katika masuala ya ushirikiano
wake na mataifa mbalimbali vinginevyo mahakama hiyo haitaweza kutekeleza
majukumu yake ipasavyo.Mkutano huo utakaoendelea hadi Alhamisi ijayo,
pamoja na mambo mengine utajikita zaidi katika masuala ya kuimairisha
ushirikiano kati ya ICC na mataifa mbalimbali.
RWANDA
Wakili adai Mugesera anatendewa kinyume na haki ndani ya jela za
Rwanda: Wakili wa mshitakiwa wa mauaji ya kimbari, Leon Mugesera adai
kuwa mteja wake anatendewa isivyo halilali ndani ya magereza ya nchi
hiyo.Wakili huyo, Jean-Felix Rudakemwa alisema malalamiko hayo ya
kukiukwa haki za msingi za mteja wake ambayo yalitumwa kwenye magazeti
nchini Canada na kuchapishwa Jumatano wiki hii ni pamoja na kutishiwa
kuuawa, kupewa chakula kilichooza na kuwepo kwa panya na papasi ndani ya
jela anamoishi.Hata hivyo wakuu wa serikali ya Rwanda wamekana vikali
madai hayo kwa kuyaita ‘’hayana maana yoyote.’’
WIKI IJAYO
ICC
Kesi ya utetezi ya Bemba kuendelea kusikilizwa: Jumatatu ijayo,
Novemba 19, kesi ya utetezi ya kiongozi wa zamani wa waasi katika
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Jean-Pierre Bemba itaendelea
kusikilizwa kwa kupata mashahidi zaidi wa utetezi.Bemba anashitakiwa kwa
uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita.
RWANDA
Mugesera kufikishwa mahakamani kwa mara nyingine: Msomi mmoja wa
Rwanda, Leon Mugesera Jumatatu ijayo, Novemba 19, atafikishwa mbele ya
mahakama mjini Kigali ili kuanza kusikilizwa kwa kesi yake