RAIS Jakaya Kikwete amezitaka
taasisi za fedha nchini kuondoa vikwazo
mbalimbali wakati wa ujazaji wa fomu
kwa ajili ya kufungua akaunti kwanye mabenki kwani
kwakufanya hivyo wananchi wanaweza kukaa na fedha majumbani badala ya kuzipeleka kwenye benki.
Aidha amezisihi benki kutoa
mikopo zaidi kwa wananchi hususan wakulima pamoja na wafugaji ili kuwa na
ongezeko kubwa la wananchi wanaojiajiri wenyewe na kupata vipato kutokana na
mikopo ya bei nafuu.
Kikwete aliyasema hayo jana
wakati akifungua mkutano wa 16 wa Taasisi za Fedha unaofanyika Jijini Arusha.
Alisema vikwazo ni vingi
katika ufunguaji wa akaunti hali inayopelekea wananchi kushindwa kufungua
akaunti na kukaa na fedha majumbani mwao na wengine kuzichimbia chini ya ardhi
kwaajili ya usalama kutokana na hatua mbalimbali za ujazaji wa fomu.
“Acheni urasimu ukitaka
kufungua akaunti mlolongo ni mkubwa sana mpaka unamchosha mwananchi anayetaka
kufungua akaunti angalie utaratibu mwingine juu ya ufunguaji wa akaunti mkiendelea hivyo mitakosa wateja pia huduma ya
utoaji wa fedha kwakutumia simu inakuwa kwa kasi kwasababu haina mlolongo mrefu
kama wa mabenki”.
Alisisitiza kuwa taasisi za
kibenki kuhakikisha zinatoa mikopo nafuu kwa wakulima na wafugaji ili
kuwawezesha wananchi kunufaika na kilimo zaidi
kwani maendeleo ya kila nchi yanatokana na kilimo cha kisasa zaidi.
Alisema hivi sasa kasi ya
utumaji wa fedha kwakutumia simu za mkononi imeongezeka zaidi na wateja wengi
wanaipenda njia hiyo kwasababu ni salama na haina mlolongo mrefu wa utumaji wa
fedha kama vile kwenye mabenki.
Naye Gavana wa Benki Kuu
(BoT), Profesa Benno Ndulu alisema Benki hiyo imezindua mfuko wa wadhamini wa
Mwalimu Julius Nyerere ambao utawezesha wanafunzi wa kike na wa kiume kupata
ufadhili wa masomo ya sayansi na hesabu
Akizindua mfuko huo wa
wadhamini ,Rais Kikwete aliipongeza benki hiyo ,taasisi za fedha pamoja na
magava wastaafu na wafanyakazi wa benki kuu kwa moyo waliouonyesha juu ya
kuendeleza elimu ambayo hayati Mwali Nyerere ambaye ni baba wa Taifa
alihamasisha sana elimu kwa vijana ambayo inaleta maendeleo.
Mkutano huo pia
ulihudhuriwa na Mama Maria Nyerere, Gavana Mstaafu, Edward Mtei pamoja na wadau
mbalimbali wa taasisi za fedha ndani na nje ya nchi.