WIZARA ya Kilimo, Chakula na
Ushirika inadaiwa kushidwa kulipa Mamilioni ya fedha za Vibarua wanaofanya kazi katika Kituo cha kueneza
Teknolojia za Kilimo ATTC, cha kanda ya Kaskazini kilicho Themi jijini Arusha
kwa miezi sita sasa.
Vibarua hao Saba wamesema hawajalipwa madai yao tangia Mwezi
marchi mwaka huu hadi sasa na hivyo wameonyesha wasi wasi kuwa huenda fedha
hizo ambazo zimetengwa kwa ajili ya malipo yao zimechachuliwa hali inayowafanya wao waishi katika mazingira
magumu na kwa matumaini kama wagonjwa wa Ukimwi ambao wajui lini watapona.
Vibarua hao wakizungumza na
vyombo vya habari katika ofisi za Idara habari maelezo, mkoa wa Arusha, wamesema
kuwa hawajalipwa Ujira wao tangia mwezi Marchi mwaka huu hivyo wao wanashindwa
kulipia kodi za nyumba, kugharimia matunzo ya familia ,kugharimia matibabu .
Wamesema kuwa wanajipanga
kukifanyia uharibifu mkubwa katika kituo hicho kutokana na kutolipwa ujira wao
kwani wamevumilia lakini sasa uzalendo umewashinda.
Kutokana na Wizara hiyo kushindwa kuwalipa kiasi cha shilingi milioni
4,200,000, wanazodai tangia Marchi hadi Novemba mwaka huu, wanaona kuwa
hawatendewi haki na kuna uwezekano fungu hilo limechakachuliwa ,na wajanja wa
wizara hiyo wasiokitakia kituo hicho mafanikio katika maonyesho ya kila mwaka
ya Nane nane.
Kituo hicho kilianzishwa na
wizara hiyo mwaka 2008 na kiliingia mkataba na vibarua hao kwa ajili ya
kuendesha Vishamba vidogo vidogo vya mafunzo ya mazao mbalimbali ya kilimo kwa
kipindi chote cha mwaka. Hivyo wakapendekeza Kituo hicho kifungwe kwa sababu
wamechoka kufanya kazi bila kulipwa kwa wakati.
”Inashangaza kila tukitaka
kulipwa lazima twende kwenye vyombo vya habari vinginevyo hatulipwi hali hii
itaendelea mpaka lini ni bora kituo hiki kifungwe vinginevyo tutafanya
uharibifu mkubwa ”, walisema vibarua
hao.
Vibarua hao wamekuwa
wakifanya kazi ya kuhudumia vipando vya mazao mbalimbali yakiwemo mazao ya
mizizi ,migomba, vikolezo na miti ya matunda.
Vibarua hao wamekuwa wakitoa
mafunzo endelevu kwa mwaka mzima kwa watu mbalimbali wanaotembelea kituo hicho
kwa kutumia teknolojia na mbinu zitakazowawezesha wakulima kulima kilimo chenye
tija na kupata faida kubwa
Vibarua hao wamesema
wanashangazwa na hatua ya Wizara hiyo kuingia mkataba na kampuni binafsi ya
Ulinzi ya SGS,kulinda Kituo hicho ,ambayo imekuwa inalipwa kila mwezi ,lakini
wao hawalipwi .
Wamesema kuwa wao wanafanya
kazi kubwa ya kutunza vipando,na na wao ndio husababisha Wizara hiyo kupata
ushindi kila mwaka katika maonyesho hayo ya Nane nane lakini hawathaminiwi licha ya mchango mkubwa wanaoutoa wa kutunza
vipando hivyo.
Msimamizi wa kituo hicho,
Elias Ernest, alipoulizwa kuhusiana na madai hayo alikiri na kueleza kuwa
ameshawasilisha Wizarani
.
Ameongeza kuwa Vibarua hao wamekuwa wakitumia lugha za
vitisho ikiwa ni kushinikiza walipwe madai yao pia wamepoteza moyo wa kufanya kazi