BREAKING NEWS

Sunday, November 18, 2012

AIRTEL LOLIONDO PICHA


Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof. Makame Mbarawa akifungua jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa radio ya jamii ya LOLIONDO FM wakati wa hafla maalum ya uzinduzi wa radio kijijini Ololosokwani. Uwekwaji wa redio hiyo ya jamii umezeshwa kwa ushirikiano kati ya Airtel na shirika lisilo la kiserikali UNESCO katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha. Kulia ni mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice Singano na wakwanza shoto muwakilishi wa UNESCO bi Vibeke Jensen

Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof. Makame Mbarawa akijaribu mtambo wa radio kwa kutangaza moja kwa moja (live) kupitia radio ya jamii LOLIONDO FM mara baada kumalizika kwa hafla ya
uzinduzi rasmi wa radio hio ya jamii iliyowezeshwa kwa ushirikiano kati ya Airtel na shirika lisilola kiserikali UNESCO katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha. Waliomzunguka wawakilishi Airtel na Unesco wakiwa na wenyeji wa kijiji cha Ololosokwani

Picha Waziri wa Sayansi Mawasiliano na Technojia Prof. Makame Mbarawa akitoa wito kwa wanafunzi na wanakijiji wa Ololosokwani kuhakikisha wanatumia vyema kituo cha mtandao wa Internet (multi media center) katika shughuli za masomo yao mara baada ya waziri huyo kuzindua mradi wa radio ya jamii LOLIONDO FM, mradi wa mtandao pamoja na kampeni ya kuwafundisha jamii ya wamasai kujenga nyumba za kisasa katika kijiji cha Ololosokwani kilichopo Loliondo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha. Waliomzunguka wawakilishi Airtel na Unesco wakiwa na wenyeji wa kijiji cha Ololosokwani

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates