CHAMA cha ununuzi na wagavi Tanzania kimejipanga kukabiliana na tatizo
la rushwa ambalo limekuwa likipelekea miradi mingi kuwa chini ya
viwango na kupelekea fedha za serikali kupotea bila kuwa na faida kwa
wananchi husika.
Hayo yamesemwa mwenyekiti wa chama cha wanunuzi na wagavi nchinin
kenya( KISIM) bw.Injini Chris Oanda wakati akizungumza katika
kongamano la kwanza la chama hicho linaloendelea mjini hapa.
Ijinia Oanda alisema kuwa swala la rushwa limekuwa ni changamoto kubwa
sana katika jamii zetu hali ambayo inapelekea miradi mingi ya serikali
kama barabara kuwa chini ya kiwango kutokana na rushwa hivyo ni
kongamano hilo litawawezesha kujadili kwa kina na kutafuta mbinu
madhubuti za kutatua changamoato hiyo.
Aidha alifafanua kuwa mpango wa ununuzi unaunganisha watu wengi zaidi
hivyo ni lazima kuwe na namna ya kuzuia rushwa kwa kuwa wanaolaumiwa
ni wasimamizi hivyo ni lazima wajisafishe kwa kutokupokea rushwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama hicho nchini Tanzania (PASAT)
bw.Nolaskus Mpota alisema kuwa lengo la kukutana ni kujadili
changamoto kubwa ya kuhusiana na viwango katika ununuzi na ugavi
kwamba wamegundua kuwa miradi mingi kutokuwa na viwango vya uhakika.
Bw.Mpota alisema kuwa ni lazima kuwe na viwango na mtu atakuwa anajua
matokeo ya kazi ambayo inafanywa hata kabla ya kazi haijaanza ili iwe
rahisi kwa mgavi ama mnunuzi kumchukulia hatua toka mwanzo au kufanya
marekebisho mapema.
Alifafanua kuwa miradi kujengwa chini ya kiwango wengi wa wazabuni
hapa nchini hawafuatilia vigezo wala hawasomi vizuri makabrasha na
kujituma kwa kuwa ununuzi ni utandawazi hivyo bila kujituma ndio kila
kitu ikiwa ni pamoja na kuzingatia vigezo.
Kongamano hilo limewashirikisha washiriki zaidi ya tisini kutoka nchi
pamoja na mashirika kama benki ya dunia,nchi kama
Nigeria,Kenya,Uganda,Marekani,Zambia na nyinginezo ambapo linatarajiwa
kumalizika rasmi octomber 19.