MZEE WA UPAKO AWAZIDI MAMLAKA YA HALI YA HEWA KW AKUTABIRI


Wakati mwingine Mamlaka ya Hali ya Hewa inawapa sifa za bure baadhi ya watu kutokana na kushindwa kwake kuwa na utabiri wa kisayansi. Itakumbukwa kuwa Mamlaka iliposema kutakuwapo mvua za El Nino, Mzee wa Upako; akatangaza kwa kuapa kabisa kwamba endapo mvua hizo zingenyesha, basi angeacha kuhubiri! Kweli, mvua hizo zimepotea, na sasa Mamlaka inathibitisha kuwa hazipo!!
Hatari ninayoiona hapa ni kwamba wananchi watakuwa na imani zaidi na wachungaji (hata kama wamo waongo) kuliko Mamlaka inayoendeshwa na wanasayansi! Pengine ni muhimu basi, Mamlaka kutofuja fedha kwa kwenda Nairobi kwenye mkutano ulioandaliwa, badala yake wamfuate Mzee wa Upako ili awaeze hiyo hali ya "hewa isiyokuwa ya kawaida" maana yake ni nini, na itakuwa na athari gani? Nashauri hiyo kwa sababu inaelekea maono yake ni zaidi ya utabiri wa wanasayansi wetu.

Haitashangaza kuona Kanisa la Mzee wa Upako likijaa hadi pomoni kutokana na "utabiri" wake huu ambao umekuwa wa kweli kuliko wa Mamlaka ya Hali ya Hewa.

Nawasilisha.

Manyerere
 

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post