Kesi ya madai inayowakabili
waliokuwa madiwani wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema leo
imehairishwa katika mahakama kuu ya kanda ya Arusha hadi hapo November 21 mwaka huu itakapo julikana hatima yao
baada ya kushindwa kulipa fidia ya zaidi ya shilingi miolini 15 .
Kabla ya kuahirisha kesi
hiyo hakimu mkazi mfawidhi ,Charles Magesa anayesikiliza kesi hiyo ,alisikiliza
hoja za pande zote mbili,ambapo wakili
wa chadema, Method kimomogoro aliitaka mahakama iwachukulie hatua kali wahusika
kwa kushindwa kulipa fedha hizo zilizoamuriwa na mahakama,April 10 mwaka
huu.
Pia akimu kimomogoro
aliiambia mahakama kwamba wadaiwa hao wamekuwa wasumbufu kwa kutaja kiwango
kidogo cha kulipa ambacho ni kinyume na vipato vyao kwani katika mahesabu ya
haraka inaonyesha kuwa kwa garama walizotaja wanaweza kulipa watatumia muda wa
zaidi ya miaka 10 hadi kumaliza kumlipa mteja wake.
“muheshimiwa hakimu huoni
kuwa kwa kila moja walivyojieliza kulipa kiasi hicho mara shilingili 15,000 kwa
mwezi na wengine 25,000 watatumia mda mrefu mno,watakuwa wanatania maakama
maana kunaambao wanawanavitega uchumi kibao huku wengine wakimiliki magari na
wengine wakimiliki magari kwanini wasiuze au kukodisha na kama tukiwasikiliza
si tutakuwa tunapotezea mda mahama “alisema kimomogoro
Kwa upande wa madiwani hao
ambao ni Charles mpanda,John bayo ,robern ngowi ,Rehema Mohamed pamoja na
Estomy Malla mmoja wa madiwani hao John Bayo akiongea mahakamani hapo alisema
kwamba hawakatai kulipa lakini watalipa kutokana na vipato vyao na kuiomba
mahakama ikubali kukubali kulipa viwango walivyovitaja.
Mara baada ya hoja za pande
zote mbili kukamilika hakimu Magesa alihairisha kesi hadi hapo November 21 (kesho
kutwa)ambapo ndipo maamuzi kamili yatatolewa.
Akiongea na waandishi wa
habari nje ya mahakama method kimomogoro alisema kuwa Awali mteja wake chadema
alipeleka mahakamani madai ya zaidi ya shilingi milini 2 9 lakini mahakama
ilichambua na kuwataka walipwe shilingi 15,116,500 huku akibainisha kuwa wao
wanasubiri mahamuzi ya mahakama apo kesho kutwa na iwapo wataamriwa walipwe
watapokea .
“sheria ya mahakama inasema
kuwa ukimpeleka mtu magereza unatakiwa umlipie hela ya chakula sasa wakishindwa
kulipa tupo tayari kuwalipia chakula ili waende kusota magereza hadi pale
watakapo lipa”alisema Kimomogoro
Aidha alibainisha kwamba
iwapo mahakama itawahukumu kifungo fedha za chakula watawalipia na kuzijumlishia
kwenye deni la mteja wake.