Wadau wakisikiliza
Shirika la Kisabato la kusaidia majanga mbalimbali ya jamii
(ADRA)mkoani hapa limefanikiwa kuwasaidia walemavu wa ngozi (ALBINO) zaidi ya
600 kutoka katika mikoa ya kanda ya kaskazini kwa kuwapa mahitaji muhimu kama vile elimu, Ajira, afya pamoja na usalama wao.
Akiongea na waandishi wa habari mapema jana katika Mkutano
wa wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa watu wenye ulemavu wa Ngozi Askofu
mkuu wa kanisa la Sabato ambaye pia ni raisi wa shirika hilo la
kisabato Dkt Edwin Lwekundayo alisema kuwa hiyo ni moja ya mikakati ya
kuhakikisha kuwa walemavu wanapata haki zao za msingi.
Dkt Edwin alisema kuwa shirika hilo limefanikiwa kuwapatia
huduma za msingi walemavu kutoka katika Mikoa ya Arusha ,Kilimanjaro, pamoja na
Tanga ambapo zoezi hilo limeanzia ngazi ya kata hali ambayo nayo imefanya
matukio mbalimbali ya uuaji wa maalbino kupungua kwa kiasi kikubwa sana tofauti
na hapo awali ambapo takwimu za mauaji zilikuwa kubwa sana.
Alifafanua kuwa huo ni mpango mkakati ambao pia ni mradi
ambao ni endelevu na utaweza kufikia katika Mikoa yote ya Nchi ya Tanzania
ambapo lengo halisi ni kuhakikisha kuwa maalbino wote wanakuwa katika hali ya
usalama zaidi ingawaje kwa sasa mpango huo umedumu kwa miaka miwili ndani ya
kanda ya kaskazini.
‘Lengo letu ni kuhakikisha kuwa maalbino wote wanakuwa
katika mpango mzuri wa kimaisha na kupitia mradi huu tutaweza kuwafikia na
kuhakikisha yale mahitaji ya msingi wanayapata kwani wengi wanakuwa katika hali
ngumu ya maisha kwa kuwa hawana muelekeo
lakini sisi tunachokiitaji ni kuhakikisha kuwa wanasonga mbele zaidi nah ii
itachangia sana hata kuweza kupunguza idadi ya vifo vya walemavu hawa’aliongeza
dkt Edwin.
Awali mgeni rasmi katika ufunguzi wa Mkutano huo George Herbert ambaye ni Naibu msajili wa mahakama ya biashara hapa
nchini alisema kuwa kwa sasa kuna mkakati hasa kwenye Kesi za walemavu wa ngozi
wa kuhakikisha kuwa zinamalizika kwa wakati
iili waweze kupata haki zao za msingi tofauti na pale ambapo kesi hizo
zinaposhindwa kumalizika kwa wakati huku hali hiyo ikichangia sana Ongezeko la
uonevu wa walemavu hao.
Herbet aliongeza kuwa pamoja na kuwa na mikakati hiyo ya kumaliza kesi za walemavu wa ngozi kwa wakati lakini bado Mahakama mbalimbali hapa nchini zinatambua na kuthamini haki za Albino hivyo nao wananchi wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanawafichua wale wote wanaosababisha madhara likiwemo suala zima la kifo kwa Maalbino.
Awali Meneja Mradi wa Shirika la Kisabato linalosaidia jamii
kwenye masuala ya majanga,Bw Soulpeace Thomas Mzee alisema kuwa kupitia kwenye
mkutano huo wa siku nne utasaidia sana kufikia
sera mkakati ambayo itaweza kuwasaidia walemavu wa Ngozi katika shuguli
zao za kila siku kupitia kwenye chama cha Maalbino Tanzania,hali ambayo itaweza
kuwapatia haki zao za ,msingi .
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia