RAIS KIKWETE AOMBEWA NA VIONGOZI WA DINI KABLA YA KUFUNGA MKUTANO WA MAJAJI LEO MKOANI ARUSHA


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiombewa dua na viongozi wa dini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa kilimanjaro leo Novemba 15, 2012 tayari kwa ziara ya siku tatu ya kikazi mkoani Arusha
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wa dini mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa kilimanjaro jioni leo Novemba 15, 2012 tayari kwa ziara ya siku tatu ya kikazi mkoani Arusha. 
 Rais Jakaya Kikwete akipokea risala ya Waheshimiwa Majaji toka kwa mwakilishi wao, Jaji Dk Fauz Twalib, wakati wa kufunga mkutano wa siku nne wa Majaji uliofanyika katika Hoteli ya Snow Crest jijini Arusha leo Ijumaa Novemba 16.
 Rais Jakaya Kikwete akifunga mkutano wa siku nne wa Majaji uliofanyika katika Hoteli ya Snow Crest jijini Arusha leo.
 Waheshimiwa Majaji wakimsikilia Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani), wakati wa kufunga mkutano wa siku nne wa Majaji uliofanyika katika jijini Arusha leo Ijumaa.
Rais Kikwete akifunga mkutano wa siku nne wa Majaji uliofanyika jijini Arusha leo Ijumaa. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Magesa Mulongo, Jaji Mkuu  Mh. Mohamed Chande Othman, Waziri wa Sheria Mh. Mathias Chikawe, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu na Jaji Kiongozi Mh. Fakih Jundu.
Rais Kikwete akifunga mkutano wa siku nne wa Majaji uliofanyika jijini Arusha leo Ijumaa. Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Magesa Mulongo, Jaji Mkuu  Mh. Mohamed Chande Othman, Waziri wa Sheria Mh. Mathias Chikawe, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu na Jaji Kiongozi Mh. Fakih Jundu.
 
 Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho kikwete Amesema kuwa lazima matatizo ya majaji yatekelezwe pamoja na kutatuliwa  ili wananchi waweze kutatuliwa matatizo yao kwa wakati
Hayo aliyasema jana wakati akifunga mkutano wa siku tano  wa waheshimiwa majaji wa mahakama ya Tanzania ulikuwa ukifanyika katika ukumbi wa hotel ya snow crest uliokuwa ukifanyika jijini hapa.
mh kikwete alisema kwamba kutekelezeka kwa masuala ya matatizo ya majaji kutasaidia kukamlika na kuandokana na na mrundikano wa mashauri ya kesi katika mahakama ze nchini
"kuukamilika ni muhimu sana maana hakuna muhimili mwingine mkubwa zaidi ya mahakama katika kupunguza mrundikano wa  kesi na mahabusu katika mahakama zetu maana ni tabu sana kusikiliza kesi na kuto maamuzi na hakuna mbadala wa  mahakama lazima tufanye kila kitu kuhusu mahakama kinachowezekana na kutekelezwa"alisema mh.kikwete
Aidha aliwataka majaji pamoja na mahakimu kuharakisha madai pamoja na kesi za watu kwani wakati mungine wao kama serekali wamekuwa wakipokea malalamiko kuwa kesi  za wananchi  hazisikilizwi kwa wakati na pia alibainisha kuwa jinsi wanavyo chelewesha kutoa mahamuzi wanachangia wananchi kuichukia serekali.

Aidha alisema kuwa kwa upande wa kujenga mahakama kuu watajitaidi kusaidia kwa muda wa miaka miwili  hadi mitatu iliyobakia kuhakikisha kuwa jengo la mahakama kuu linapatikana na sio hilo tu pia watajitaidi kila mkoa kuwa na jengo lake jipya ambalo litatumika kama mahakama kuu.
Akitoa shukurani mbele ya raisi mh jaji January Msofe alisema kuwa wao kama majaji watahakikisha wanatatua matatizo ya wanachi kwa wakati maana wao kama mahakama ni jukumu kubwa kwao kusikiliza na kujadili matatizo yote yanayoletwa kwao na kuahidi kufanya kwa ufanisi na kuahidi pindi mahitaji hayo yatakapokamilika kutapunguza mrundikano wa kesi na maadili na nidhamu  kwa majaji yatazingatiwa .

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post