UADILIFU WA KINANA WAANZA KUTIA SHAKA.
Posted by
woinde
on
Monday, November 19, 2012
in
|
KATIBU MKUU MPYA WA CCM ABDULRAHMAN KINANA
-
NI UTAJIRI WAKE WA KUPINDUKIA.
-
ATAJWA KATIKA SAKATA LA USAFIRISHAJI WA MENO YA TEMBO.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, ambaye
maisha yake kwa muda mrefu yamekuwa ayamulikwi na waandishi wa habari
safari hii yameanza kuingia dosari baada ya kutangazwa rasmi kuwa Katibu
Mkuu CCM.
Gazeti
moja la wiki ndilo lililokuwa la kwanza kwa kuchapisha habari
iliyomueleza kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni iliyousika na
usafirishaji wa meno ya tembo.
Duru
nyingine za mambo ya siasa sina muusisha na utajiri uliyo kithiri
pamoja na uhusianao wa moja kwa moja na Kampuni ya Kiarubu iliyoipewa
sehemu ya Loliondo Kuwinda ambayo inapigiwa kelele na wanaharakati mpaka
leo hii.
Binafsi Katibu Mkuu huyo wa chama tawala amesema hahusiki na usafirishaji wa meno ya tembo nje ya nchi.
Hata
hivyo, amekiri kuwa mmiliki wa Kampuni ya uwakala wa meli ya Sharaf
Shipping Agency, iliyohusika kusafirisha makontena yaliyokuwa na nyara
hizo za serikali, kabla ya kukamatwa nchini China yakiwa safarini
kupelekekwa Hong Kong.
Gazeti
hilo lilimtaja Kinana kuwa mmoja wa wamiliki wa kampuni hiyo kwa kuwa
na hisa 7,500 kati ya 10,000 katika kampuni hiyo, huku hisa nyingine
2,500 zikiwa zinamilikiwa na mshirika mwenzake, Rahma Hussein. Thamani
ya hisa hizo ni sh 1,000 kila moja.
Kinana akitoa ufafanuzi kuhusiana na hilo alishanga kuhusishwa na meno hayo.
“Nimeisoma habari hiyo na kwa
bahati mbaya sioni anayenilaumu wala kitu ninacholaumiwa nacho. Kwamba
nina hisa katika kampuni ya wakala wa meli ya Sharaf ni kweli.
“Lakini
mimi sina nafasi yoyote ya kiutendaji na wala sishughuliki na
uendeshaji wa kampuni hiyo. Kwa kweli sikujua na wala sikuhusika kwa
namna yoyote ile na usafirishaji wa makontena hayo na mengine yoyote,”
alisema Kinana.
Alifafanua
kuwa, wenye wajibu na mamlaka ya kukagua shehena zote zinazosafirishwa
nje ya nchi ni mamlaka za serikali na si kampuni ya uwakala wa meli.
Alisisitiza
kuwa, hana mamlaka kwa mujibu wa sheria kukagua mali inayosafirishwa
japokuwa anaweza kuuliza bidhaa iliyopo katika makontena hayo.
“Ni dhahiri kabisa kwamba,
habari hii imeandikwa na jina langu kutumika katika malengo ambayo
siyajui. Nahisi kama jina langu limetumika kama pilipili katika
kachumbari ili kunogesha habari.
“Kwa
bahati mbaya pilipili imezidi katika kachumbari. Kama lengo lilikuwa
kupasha habari, basi umma umedanganywa,” alisema Kinana.
Kwa mujibu wa habari hiyo,
sakata la kukamatwa kwa nyara hizo za serikali liliibuliwa kwa mara ya
kwanza na Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela, katika
Bunge lililopita la bajeti.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia