TAMASHA LA KUCHANGIA MTOTO WA KIKE LAFANYIKA NCHINI UINGEREZA


 
Mama Joyce Kallaghe Akipakwa Hina kwa ajili ya kuchangia Mfuko wa elimu
Mama Joyce Kallaghe ambaye ni Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Commonwealth Countries League (CCL) walioandaa Tamasha la Kuchangia Mtoto wa Kike akiwaonyesha wageni mbali mbali vitu tofauti tofauti vitakavyouzwa kwa ajili ya kuchangia mfuko huu.
Mama Kiondo akiwa kikazi zaidi kuitangaza Tanzania.
Mayorese Mrs. Anne Hobson katika banda la Tanzania.
Mstahiki Meya akiangalia sehemu ya vyakula vya Tanzania.
kutoka Kushoto Mh balozi wa Grenada Ruth Elizabeth Rouse, Mtahiki Meya Christopher Buckmaster na Mama Balozi Joyce Kallaghe.
Mama Balozi akimkabidhi Mayorese Mrs. Anne Hobson baada ya kununua kitenge katika banda la Tanzania.
Sherehe ikiendelea.
Ukumbi wa Royal Borough of Kensington.
wateja wakinunua bidhaa kutoka banda la Tanzania.
 
 
Meya wa Manispaa ya Royal Kensington na Chelsea nchini Uingereza,Christopher Buckmaster akizungumza wakati wa kufungua Tamasha la Kuchangia Mtoto wa Kike lililofanyika Royal Borough of Kensington chini ya uongozi kutoka kwa Mh. Balozi wa Grenada Ruth Elizabeth Rouse ambaye ndio raisi wa Jumuiya hiyo akisaidia na Makamu wake Mama Joyce Kallaghe ambaye ni Mke wa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza,Mh. Peter Kallaghe.

Salam,

 Jumuiya ya Commonwealth Countries League (CCL) inayoshirikisha nchi hamsini na nne (54) duniani kutoka katika jumuiya ya madola iliandaa tamasha maalum siku ya jumamosi tarehe 3.11.12 kwa ajili ya kuchangia mfuko wa kumsaidia na kumwezesha msichana kusoma elimu ya sekondari.

 Historia ya Commonwealth Countries League ilianzishwa rasmi kutoka kwa baadhi ya wanawake mnamo mwaka 1923 nchini Australia kwa ajili ya kusaidia kutangaza uelewa wa haki sawa kati ya wanawake na wanaume waliopo nchi mbalimbali zilizo ndani katika jamuiya ya madola.

 Tamasha hili lilifanyika Royal Borough of Kensington chini ya uongozi kutoka kwa Mh. Balozi wa Grenada Ruth Elizabeth Rouse ambaye ndio raisi wa jumuiya hiyo akisaidia na makamu wake mama Balozi Joyce Kallaghe.

Wageni Rasmi walikua Wastahiki Mameya wa Worshipful Royal Borough of Kensington na Chelsea - Councillor Christopher Buckmaster na Mrs. Anne Hobson Shughuli ya mwaka huu iliandaliwa na wake za mabalozi kutoka katika jumuiya za Madola hamsini na nne (54) ili kuchangisha pesa kwa njia ya kuuza vitu mbalimbali vya asili kama chakula, urembo, maua, vinywaji n.k.

Fedha zote zilizopatikana zilipelekwa kusaidia mfuko huu wa Elimu kwa ajili ya kumsomesha mtoto wa kike. Aidha Mama Balozi Joyce Kallaghe aliongeza kwa kusema ''Elimu ni Ufunguo Wa Maisha kumsomesha mwanamke ni kuiwezesha jamii nzima hivyo vipaumbele vyote vimeelekezwa kwa kwa ajili ya kuwasomesha watoto wa kike walio maskini au wanaoishi katika mazingira magumu ambao wana uwezo wa kuendelea kusoma elimu ya sekondari katika nchi za jumuiya ya Madola".

Tangu mwaka 2011/2012 mfuko wa Elimu wa CCL ushawawezesha watoto wa kike 364 kutoka nchi 25 ikiwapo Tanzania. Pia aliwasihi wadau kuwa wazalendo kwa kuchangia mfuko huu kwa kuwasiliana kupitia barua pepe ccl.edfund@googlemail.com Kiasi cha paundi mia moja hamsini (£150) na Mia nne na hamsini (£450) zinatosha kumsomesha msichana kwa mwaka mzima

 Asanteni

 Urban Pulse Creative
 

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post