BUNGE FC YAJICHUA VILIVYO KWA AJILI YA MASHINDANO YA MABUNGE YATAKAYOFANYIKA NCHINI KENYA



Picha ikionyesha naibu waziri wa elimu Tamisemi Kassimu Majaliwa ambaye ni kocha wa timu ya Bunge FC akiwapa somo wachezaji wakati wa mazoezi katika uwanja wa kumbukumbu ya sheikh amri abeid

Na Woinde Shizza,Arusha
Timu ya bunge Fc  imejipanga kunyakua ubingwa wa mashindano  ya mabunge inayotarajia kuanza kutimua vumbi mapema mwezi december mwaka huu.
Akiongea na  waandishi wa habari  mwenyekiti  timu  hiyo  ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Kinondoni Idd Azan alisema kuwa timu yake imejipanga vilivyo kwa ajili ya kunyakuwa ushindi katika mashindandano ya timu za mabunge ya jumuiya ya afrika mashariki yanayotarajia kunyika nchi jirani ya kenya.
Alisema kuwa mpaka sasa wachezaji wote wapo katika mazoezi ambapo alibainisha kuwa mazoezi hayo yanafanyiwa katika uwanja wa sheikh amri abeid jijini hapa kwa muda wa wiki mbili.
Azan alisema kuwa katika mazoezi yao wanatarajia kucheza mechi za kirafiki ambapo alibainisha kuwa mpaka sasa wanatarajia kucheza na timu ya Ngorongoro conservation  mbayo mechi hiyo itachezwa ndani ya hifadhi.
Kwa upande wake kocha wa timu ya Bunge FC Naibu waziri wa elimu tamisemi Kassim Majaliwa alisema kuwa kuwa kikosi chake kiko vizuri na maandalizi yamekamilika na wanaimani watashinda.
"kwa mazoezi ninayowapa timu yangu ninauhakika mwaka huu tunaleta ubingwa tanzania na kunamazoea ya kuwa mashindano yakifanyikia katika nchi fulani wenyeji ndio wanachukuwa kombe kwa mwaka huu tunabadilisha usemi huo lazima tuje na matokeo"alisema Majaliwa
Adha aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia mazozi yanayoendelea jijini arusha kwa muda wa wiki mbili katika uwanja wa sheikh amri abeid jijni hapa.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post