bwana Bill Mushi akihutubia kwenye mahafali hayo |
Waandishi wa habari
wametakiwa kuandika suluhisho ya matatizo mbali mbali yanayoikumba jamii ya
watanzania na siyo kila siku kukazania kuandika tu mapungufu yanayosemwa juu ya
viongozi wa serikali.
Rai hiyo imetolewa na bwana
Bill Mushi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwenye mahafali ya tano ya
chuo cha uandishi wa habari na utangazaji (AJTC) kilichopo mbauda mkoani
Arusha.
Bwana Bill alisema kuwa mara
nyingi waandishi wa habari hupenda zaidi kuandika mapungufu mbali mbali
yanayojitokeza kwa viongozi wetu na kuwa changamoto kwa jamii bila kujali
sababu hali ambayo imekuwa kikwazo kwa baadhi wa watendaji na kushindwa kufanya
kazi kwa ufanisi zaidi.
“ Kweli kuna changamoto
nyingi zinazoikumba jamii hasa ajira kwa vijana, lakini si vema kukazania
kuandika kuwa kuna tatizo la ajira, ni lazima mda mwingine make na kufikiri
nini cha kuandika ambacho kitakuwa ni suluhu la tatizo hilo”Alisema Bill.
Pia aliwataka kutoandika
zaidi habari za kuripoti badala yake wajikite zaidi katika habari za
kiuchunguzi ili kuisaida nchi yetu kujua mambo mengi mtakayoyaibua ikiwemo
kuibua vyanzo mbalimbali za mapato katika jamii.
Naye mkurugenzi wa chuo hicho
cha Arusha Journalism Trainning College (AJTC) Bwaba Joseph Mayagila alisema
kuwa wahitimu hao 75 wamemaliza kozi tofauti tofauti ikiwemo cheti cha juu cha
uandishi wa habari, stashahada, na stashahada ya juu ya uandishi wa habari
pamoja na uhusiano wa kimataifa.
Pia Mayagila aliongeza kuwa
tofauti na kozi hiyo iliyowafanya wanafunzi hao kuja chuoni hapo pia wanatoa
elimu ya ujasiriamali itakayoweza kuwasaidia wahitimu kukabiliana na tatizo la
ajira wakiwa mitaani ikiwemo kutokuangalia zaidi kuajiriwa badakla yake wabuni
vyanzo vyao wenyewe vya mapato na wajiajiri kiujasiriamali.
Chuo hicho pekee chenye kutoa
mafunzo ya hali ya juu ya uandishi wa habari na utangazaji inayoendana na soko
la jumuiya ya Afrika mashariki pia inatoa mafunzo ya kompyuta, ujasiriamali na
kukuza fani mbali.
Baadhi ya wahitimu wakiwa na nyuso za tabasamu baada ya kuhitimu mafunzo |
Katika burudani: AJTC mamong'o pia wapo |