PANAAFRICA ENTERPRISE YASHEREKEA NA WAFANYAKAZI WAKE WA MKOA WA ARUSHA MIAKA MITANO YA KUANZISHWA



Kampuni ya magodoro ya Panaafrika enterprise leo limekutana na wanafanyakazi wake wa mkoani Arusha kusherikia miaka mitano tangu kuanzishwa kwa tawi la kampuni hiyo lililopo jijini hapa.

Akiongea katika sherehe hizo meneja masoko  wa kampuni hiyo Rumin Shah alisema kuwa wamaeamua kusherekea kwa pamoja sikukuu hii ya kuanzishwa kwa tawi hili la mkoani hapa ili kujipongeza kwa pamoja shughuli walioifanya hadi kufikia jijini hapa.

Alisema kuwa mpaka sasa kampuni hiyo ya magodoro imeshaajiri wafanyakazi 1500 kwa mkoa wa Arusha na wanampango wa kuendelea kuajiri wafanyakazi wengi zaidi.

Aidha alisema kuwa mbali na hivyo wanampango pia wa kufungua viwanda vingi zaidi katika nchi za jumuiya ya Afrika mshariki na sasa ivi wameanza mchakato wa kufungua kiwanda nchini Rwanda,burundi pamoja na kenya.

Adha alisema kuwa kampuni yao inampango wa kuajiri wafanyakazi wengi zaidi wa katanzania kwani nia halisi ya kampuni yao ni pamoja na kutoa ajira kwa vijana wengi wa kitanzania

Kampuni hii ya Panaafrika enterprise inashulika na mambo mbalimbali ikiwemo utengenezaji wa magodoro ya comfly lala fofo.

Alitoa wito kwa wanachi wa jumuiya ya afrika mashariki kutumia magodoro haya kwani magodoro haya ni ya uhakika na yanauboro wa kutosha nhuku akitoa taadhari ya wananchi wanaonunua kuwa makini kwani wasidnunue godoro lisilikuwa na alama ya garantii

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post