WADAU
mbalimbali wa benki
ya NMB mkoani Arusha wameiomba benki hiyo kuanzisha utaratibu wa
kuwakopesha
wateja wake nyumba za gharama nafuu ili kuwanufaisha na mikopo
wanayokopa katika benki hiyo hususani wajasiriamali wenye kipato kidogo.
Pamoja na kuwa benki hiyo
imekuwa ikitoa mikopo ya aina mbalimbali kwa wateja wake , hali hiyo
imewawezesha kuwaondoa katika wimbi la umaskini
kwa kuanzisha miradi midogomidogo, ila kwa upande wa nyumba imekuwa ni
changamoto kubwa kwao kwani bado benki hiyo haijaweza kuwasaidia .
Hayo yalielezwa na wafanyabiashara
wananchama wa klabu ya NMB (NMB business club,)mkoani hapa,wakati
walipohudhulia mafunzo ya pili ya siku
moja ya ujasiriamali yanayotolewa na benki hiyo kupitia virabu vya
wajasiriamali vya NMB,ambapo mwaka huu yanayolenga kujua faida na athari za
ushindani katika biashara zao yaliyofanyika
jijini hapa.
Alisema kuwa, asilimia
kubwa ya wadau wa benki hiyo wamekuwa wakichukua mikopo kwa ajili ya kuboresha
biashara zao ila wengi wao bado hawajaweza kujenga nyumba nzuri za kuishi
hususani wenye vipato vya chini, hivyo endapo benki hiyo itaanzisha mchakato wa
kuwajengea na kuwakopesha nyumba za bei nafuu wataweza kuwasaidia kuondokana na
changamoto hiyo.
‘Kwa kweli benki hii
imekuwa ikitusaidia sana sisi wajasiriamali katika kuhakikisha tunajikwamua na biashara na kuweza kuondokana na changamoto
mbalimbali za kimaisha , hivyo endapo watatujengea nyumba hizo za bei nafuu
tutaweza kuishi maisha yaliyo bora zaidi’alisema
Amina.
Aidha waliiomba benki hiyo
,kuanzisha huduma za viza kama wanavyofanya benki nyingine ili kuwawezesha
kuchukua fedha hata wawapo nje ya nchi
ili kuweza kufanya bishara zao kwa uhakika zaidi wawapo nje ya nchi.
Akifungua mafunzo hayo ,
Meneja wa benki hiyo kanda ya kaskazini Vicky Bishubo alisema kuwa benki hiyo imeboresha huduma ya mikopo kwa wajasirimali kwa kiwango
kikubwa kutoka shilingi milioni 1 na milioni 5 hadi kufikia sh, milioni 10 ,
hatua ambayo alisema itamsaidia mfanyabiashara mdogo kuongeza biashara zake na
kujitanua zaidi.
Alisema kuwa , mafunzo hayo
ambayo yamekuwa yakitolewa mwaka hadi mwaka yamekuwa yakiwawezesha wajasirimali
hao kuboresha biashara zao ikiwa ni
pamoja na kubuni biashara mpya zenye tija ambazo zimewawezesha kujikwamua
kiuchumi.
Bishubo alitaja malengo ya
mafunzo hayo ni kuwawezesha washiriki kupata magfunzo ya msingi ya usimamizi wa
biashara ,kuwawezesha washiriki kuelewa maana ya ujasirimali na kupata mbinu za
kufanikisha biashara ba kuiendeleza ,pamoja na kuwawezesha kuwa na ujasiri wa kuchukua mikopo.
Naye Mkuu wa kitengo cha
wajasiriamali , Filbert Mponji alisema kuwa,benki hiyo imejiwekea mkakati
ifikapo mwaka 2013 kuanzisha akaunti ya biashara kwa wajasirimali
itakayowawezesha kuchukua fedha wakati wowote wanapohitaji.