BABA ASKOFU NJOMBE AWATAKA WANANDOA KULEA FAMILIA ZAO NA KUKEMA VIKALI NDOA ZA JINSIA MOJA

Muhasham Baba Askofu wa Jimbo Katholiki Njombe  Alfred Maluma
Amekemea Ndoa za Jinsia Moja na Kuwataka Wanandoa Kuzilea Familia Zao
Katika Maadili  Mema na ya Kumpendeza Mwenyezi Mungu Kwa Kuanzia Ngazi
ya Wanandoa Hadi Watoto.

Muhasham Baba Askofu Maluma  Ameyasema HayoKatika Kilele cha
Maadhimisho  ya Kitaifa ya Jumuiya ya Wanandoa Ambapo Amelezea Hali ya
Mwenendo wa Ndoa Nyingi Kuanza Kubadalika Huku Baadhi ya Matifa
Yakiziomba Seriakli Zao na Kuidhinisha Ndoa za Jinsia Moja.

Aidha Muhasham Baba Askofu  Maluma Amewataka Wanandoa na Jamii Kwa
Ujumla Kuwalea Watoto Katika Maadili ya Kiafrika na Kuwatahadharisha
na Tamaduni za Nchi za Magharibi Ambazo Haziendani na Tamaduni ya
Kiafrika na Kuongeza Kuwa Nguzo Muhimu Kwa Wanadoa Ambazo Wanapaswa
Kuzidumisha ni Pamoja na Upendo na Ukarim Katika Familia Zao.

Akizungumzia KushukaKwa Maadili Kwa Kizazi cha Sasa Muhasham Baba
Askofu Maluma Kwa Kiasi Kikubwa Kinachangiwa na Udhaifu wa Wazazi Ama
Walezi Kutokana na Wazazi Hao Kupenda Mambo ya Kisasa Pamoja na
Utandawazi.


Akizungumza Mara Baada ya Kumalizika Misa Takatifu ya Wanandoa
Mwenyekiti wa Wanandoa Waliobarikiwa Kanisani Bwana Ventura Mwinuka
Amesema Maadhimisho Hayo Yamenzinduliwa Novembe Mbili Mwaka Huu
Katika Parokia ya Kisinga Wilayani Makete na Kilele Chake Kimefanyikia
Leo Jimbo la Katholiki Njombe.

Maadhimisho Haya ya Miaka 27 ya Wanandoa Yamewakutanisha Majimbo
Mablimbali ya Kanisa Hilo Yakiwema Majimbo ya Mwanza , Iringa , Moshi
na Songea.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post