Mkuu
wa Polisi wilaya ya Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Gilles
Muroto akifafanua jambo wakati wa mkutano wa Ulinzi shirikishi
uliofanyika katika shule ya Msingi Sokoni One iliyopo katika jiji la
Arusha. mkutano huo uliofanyika tarehe 12.11.2012 uliwajumuisha askari
wa jeshi la Polisi, viongozi wa kata ya Sokoni one na askari wa vikundi
vya Ulinzi shirikishi
Mkuu
wa kitengo cha Polisi Jamii mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi (SP) Mary
Lugola akitoa elimu ya Polisi Jamii kwa askari wa vikund vya ulinzi
shirikishi katika mkutano uliofanyika shule ya Msingi Sokoni One iliyopo
kata ya Sokoni One jijini Arusha juzi tarehe 12.11.2012
Maofisa
wa Jeshi la Polisi waliokaa kutoka kushoto ni Mkuu wa Polisi wilaya ya
Arusha (SSP) Gilles Muroto, Mkuu wa kitengo cha Polisi Jamii mkoa wa
Arusha (SP) Mary Lugola na Mkuu wa kituo cha Unga Limited (SSGT) Shaban
Shaban wote kwa pamoja wakimpongeza kwa kumpigia makofi afisa Mtendaji
wa Kata ya sokoni One Bw.Gustafu Milambo(Aliyesimama) kutokana na kazi
nzuri anayeifanya kwenye kata yake juu ya uanzishwaji wa vikundi imara
vya polisi Jamii.
Baadhi
ya kikundi cha polisi Jamii cha mtaa wa Kanisani katika kata ya Sokoni
One wakisikiliza kwa umakini elimu ya Ulinzi shirikishi iliyokuwa
inatolewa na Maofisa wa Jeshi la Polisi mkoani hapa. Mkutano huo
ulifanyika juzi tarehe 12.11.2012 katika shule ya Msingi Sokoni One
iliyopo jijini Arusha