Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi akizungumza na Waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Uingereza na Mbunge wa Jimbo la South Shields Mh.David Miliband wakati ujumbe wa TTB ulipotembelea Uwanja wa Sunderland FC na kushuhudia mchezo wa ligi kuu ya Uingereza kati ya timu hiyo na timu ya Aston Villa uliofanyika siku ya jumamosi nchini Uingereza, Bodi ya utalii Tanzania inatangaza matangazo ya utalii wa Tanzania katika viwanja sita vinavyotumika kuchezea ligi kuu ya Uingereza (Premier Liegue) kikiwemo kiwanja cha Sunderland FC, katika picha katikati ni Edmund Hazal Mkurugenzi wa Kampuni ya Lantech Services inayoratibu matangazo hayo,Bw. David Miliband pia ni mwenyekti wa klabu ya Sunderland. Waziri wa mambo ya nje wa zamani wa Uingereza na Mbunge wa Jimbo la South Shields Mh.David Miliband akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Bw. Geofrey Meena kushoto mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa ligi kuu ya Uingereza kati ya Suderland na Aston Villa, David Miliband pia ni mwenyekiti wa klabu ya SuderlandMkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB Devotha Mdachi akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa zamani na maafisa wa timu ya Sunderland FC baada ya kukabidhiwa zawadi ya saa kutoka kulia ni Balozi wa Sunderland na Golikipa wa zamani Jimmy Montgomery, Gary Mutchinson Mkurugenzi wa Biashara na Kevin Ball Nahodha wa zamani wa timu hiyo.Balozi wa Sunderland na Golikipa wa zamani Jimmy Montgomery kiutambulisha ujumbe wmaafisa wa bodi ya utalii TTB ulipotembelea uwanja huo.
Ujumbe
wa Bodi ya Utalii Tanzania TTB akipiga picha ya pamoja na wachezaji wa
timu ya Sunderland katika hafla hiyo wa pili kutoka kulia waliosimama
nyuma ni James MacFadden wa nne ni David Meyler na wa sita ni Titus
Brambie.Hapa ndiyo lango kuu la kuingilia kwenye jukwaa kuu la uwanja huo
Ujumbe
wa Bodi ya Utalii na maafisa wa taasisi mbalimbali wakipiga picha ya
pamoja nje ya uwanja huo kutoka kulia ni Bw. Manase kutoka Ngorongoro,
Bw. Mukhtar kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki , Mkurugenzi wa Masoko
TTB Devotha Mdachi, Geofrey Meena Meneja Masoko TTB na Edmond Hazal
Mkurugenzi wa kampuni ya Lantech Services inayoratibu matangazo hayo
katika viwanja vya ligi kuu Uingereza.
Ujumbe wa Bodi ya Utalii ukiwa katika picha ya pamoja na mwenyeji wao Mkurugenzi wa Biashara wa Sport Five Tony Davison.
Kutoka
kulia ni Bw. Manase, Geofrey Meena, Mukhtar na Devotha Mdachi wakiwa
wamekaa katika moja ya maeneo ya benchi la ufundi uwanjani hapo.
Meneja
masoko wa Bodo ya Utalii akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Masoko wa
Bodi hiyo Devotha Mdachi wakati walipotembelea uwanjani hapo jumamosi
iliyopita , katikati ni Bw. Mukhtar wa (EAC) nBw. Manase kutoka hifadhi
Ngorongoro.
Kutoka
kulia ni Tony Davison, Geofrey Meena, Edmond Hazal na Devotha Mdachi
wakifurahia jambo wakati mchezo huo ukiendelea kati ya Sunderland na
Aston Villa.
Matangazo ya Utalii wa Tanzania yakipita katika lininga maalum za matangazo uwanjani hapo kama yanavyoonekana.
Matangazo ya Utalii wa Tanzania yakipita katika lininga maalum za matangazo uwanjani hapo kama yanavyoonekana.
Hapa wakigonganisha glasi kutoka kulia ni Geofrey Meena, Devotha Mdachi, Tony Davison na Moses Mwangi.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia