Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo juu ya ukarabati wa ukumbi wa mikutano wa 'White House' ulio katika makao makuu ya CCM mjini Dodoma ambao unafanyiwa ukarabati mkubwa ili kukidhi mahitaji ya sasa. Rais Kikwete alisimama kwa muda mjini Dodoma siku ya Jumanne Novemba 6, 2012 akitoka katika ziara ya kikazi mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Singida alikokagua jumla ya miradi 19 ndani ya wiki moja.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete
akikagua maandalizi ya ukumbi utaotumika wakati wa mkutano Mkuu wa CCM
ulio kitongoji cha Kizota mjini Dodoma. Rais Kikwete alisimama kwa muda
mjini Dodoma siku ya Jumanne Novemba 6, 2012 akitoka katika ziara ya
kikazi mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Singida alikokagua jumla
ya miradi 19 ndani ya wiki moja.
Mafundi rangi wakiwa kazini kuweka mambo sawa nje ukumbi utaotumika
wakati wa mkutano Mkuu wa CCM ulio kitongoji cha Kizota mjini Dodoma Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete na viongiozi wengine wakipata maelezo toka kwa Katibu Mkuu wa CCM Bw. Wilson Mukama juu ya maandalizi ya ujenzi wa makao makuu na vitega uchumi wa chama hicho mjini Dodoma ambako alisimama kwa muda siku ya Jumanne Novemba 6, 2012 akitoka katika ziara ya kikazi mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Manyara na Singida alikokagua jumla ya miradi 19 ndani ya wiki moja.