JK AMJULIA HALI SHEIKH ALIYEMWAGIWA TINDIKALI ZANZIBAR


 Rais Jakaya Kikwete akimjulia hali na kumpa pole Katibu wa Mufti wa Zanzibar, Sheikh Fadhili Soraga ambaye amelazwa katika chumba cha dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kufuatia majeraha ya usoni na kifuani yaliyotokana na  kurushiwa Tindikali na watu wasiojulikana wakati akifanya mazoezi katika Kiwanja cha Mwanakwerekwe mjini Unguja juzi. Rais ambaye amerejea  jana Jumanne, akitokea katika ziara ya kikazi ya  takriban juma moja katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida, amemtakia Sheikh Soraga nafuu ya haraka. (PICHA NA IKULU)

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.