Ticker

6/recent/ticker-posts

WATU WANAOSADIKIWA KUWA NI WANAJESHI WASHIKIOLIWA KWA TUHUMA ZA WIZI



JEshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia  watu 10 wanaosadikiwa kuwa ni askari wa jeshi la wananchi  (JWTZ) kikosi cha 44 Kj  kambi ya mji mdogo wa Mbalizi  kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya kijana  Petro Sanga(25)  kwa kumchoma kisu shingoni na mdomoni na  wengine sita kujeruhiwa  kwa kumshambulia kwa kipigo.

Taaarifa iliyotolewa katika vyombo vya habari na Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya Diwani Athuman zilieleza kuwa  tukio hilo lilitokea  novemba 18 majira ya 3.00 za usiku  ambapo marehemu alikuwa akipata kinywaji  katika baa ya power night club.


“Awali marehemu alikuwa akipata kinywaji katika  baa hiyo na kwamba walivamia na kuanza kuwashambuliwa wananchi waliokuwepo  akiwemo marehemu ambaye alipingwa sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia mateke,mikanda,marungi,sime na mapanga na  kisha kumchoma kisu na kwamba marehemu alijaribu kujiokoa kwa kukimbilia baa iitwayo vavenemwe “Alisema Diwani.


Awali diwani alisema mara marehemu baada ya kupoteza fahamu  na kukimbizwa katika hosptali teule ya ifisi iliyopo  katika mji mdogo wa mbarizi  alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa vibaya  na kuvuja damu nyingi.


Diwani alisema kuwa uchunguzi umebaini kuwa chanzo  cha vurugu hizo na  kushambulia wananchi kwa kipigo na kusababisha kifo ni kutokana na  askari wa jeshi Geodfery Matete (30)  kushambuliwa na walinzi wa kilabu cha pombe za kienyeji  kilichojulikana kwa jina la (DDC) novemba 17 mwaka huu

.Alisema kuwa   kufuatiwa tukio hilo la kushambuliwa kwa mwanajeshi  lilipelekea jeshi la polisi kuwashikilia walinzi wanne kwa mahojiano zaidi na aliwataja  kuwa ni Frenk Mtasimwa(25) Mure Julius (26) Omari Charles (28) na Regnad Mwampete wakazi wa izumbwe mbeya vijijini.

Diwani   alisema kuwa majina ya watuhumiwa hao yatatajwa baadaye kwani bado uchunguzi unaendelea na kwamba ametoa wito kwa vyombo vya dora kutojichukulia sheria mikononi kwa kufanya vurugu bila kujari madhara yanayojitokeza hususan kuharibu mali hususan magari kwa kuvunja vioo na kwamba uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani.


Aidha alisema kuwafutia tukio hilo  jeshi la polisi linafanya jitihada za dhati kwa mujibu wa sheria ili haki itendeke na kutoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kwa jeshi la polisi pindi matukio hayo yanapotokea.
 Hawa Mathias,Mbeya.
 

Post a Comment

0 Comments