BREAKING NEWS

Monday, November 5, 2012

RAIS KIKWETE KATIKA ZIARA YAKE MKOANI ARUSHA NA MANYARA

 Rais kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wahabari wa mkoa wa Arusha
 Rais Kikwete akisalimiana na baadhi ya wananchi wa  mkoa wa Arusha baada ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Arusha Minjingu maene ya kijiji cha Mguu-wa-Zuberi wilayani Monduli, Mkoani Arusha.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) Mhe Rose Kamili baada ya kuzindua mradi mkubwa  wa maji  wa Mwakonko Singida Mjini.


 Rais kikwete akisalimia na mdada wa libeneke la kaskazini mara baada ya uzinduzi wa barabara ya Arusha -Minjingu
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Tonia Kandiero na viongozi wengine wakikata utepe  kuzindua barabara ya Minjingu-Babati-Singida nje kidogo ya mji wa Babati Mkoa wa Manyara. Anayeshuhudia kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt John  Pombe Magufuli na kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji) Dkt Mary Nagu


 Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier akipanda mti kama kumbukumbu baada  ya  Rais Kikwete kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Arusha Minjingu maene ya kijiji cha Mguu-wa-Zuberi wilayani Monduli, Mkoani Arusha.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Tonia Kandiero na viongozi wengine wakikata utepe  kuzindua barabara ya Minjingu-Babati-Singida nje kidogo ya mji wa Babati Mkoa wa Manyara. Anayeshuhudia kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt John  Pombe Magufuli na kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwezeshaji) Dkt Mary Nagu
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe Frederick Sumaye wakati wa mkutano wa hadhara mjini Katesh mkoani Manyara
Rais Kikwete akisalimiana na baadhi ya wanahabari wa mkoa wa Arusha baada ya kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa barabara ya Arusha Minjingu maene ya kijiji cha Mguu-wa-Zuberi wilayani Monduli, Mkoani Arusha

 RAISI  wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania dkt Jakaya Kikwete,amesema
kuwa ili Nchi ya Tanzania iweze kukua  katika viwango vya nchi ambazo
zinaendelea Ulimwenguni ni lazima ihakikishe kuwa kwanza inawekeza
zaidi kwenye maendeleo ya Sayansi na Teknolojia

Dkt Kikwete aliyasema hayo mapema jana wakati wa uzinduzi wa chuo cha
Sayansi na Teknolijia cha Nelson Mandela(NM –AIST)kilichopo Tengeru
Mkoani hapa

Aidha alisema kuwa ni wazi kuwa hakuna nchi yoyote ambayo inaendelea
au inayotaka kuendelea na kuondokana na Umaskini na lazima kwanza
kutoa kipaumbele kwa masuala ya Sayansi na Teknolojia hivyo Tanzania
inatakiwa kuhakikisha kuwa inajikita zaidi katika kuzalisha
wanasayansi walio wengi na bora zaidi ili kuharakisha zaidi maendeleo

Alifafanua kuwa endapo kama Nchi ya Tanzania itaweza kuzalisha
wanasayansi wengi sana basi itaweeza kuweka historia mbalimbali
duniani huku wanasayansi hao pia watachangia sana hata kuboresha sana
maendeleo ya nchi na hatimaye kufikia nchi za  Ukanda wa Afrika.

“Serikali ina wajibu wa kuhakikisha kuwa suala zima la sayansi
linakuwa kwa kiwango cha Kimataifa na ndio maana tuko Tayari kuchangia
ili hiki chuo cha Nelson Mandela kiweze kutufanya kuwa na wanasayansi
wengi sana ambao watabadilisha mtizamo wa nchi Yetu pamoja na kufanya
chuo hiki kiwe ni moja ya chuo ambacho kimetukuka sana barani
Afrika’aliongeza Dkt Kikwete

Katika hatua nyingine alisema kuwa Serikali itahakikisha kuwa inatoa
Kipaumbele na kutenga bajeti ya Utafiti hasa katika masomo ya Sayansi
na Teknolojia ambapo   hatua hiyo itaweza kuwaraisishia wataalamu hao
kuweza kufanya Tafiti zao ndani na nje ya Nchi na hatimaye kufikia
malengo yao pamoja na Serikali

Kutokana na hilo alisema  Serikali itahakikisha kuwa inatenga kiasi
cha Asilimia moja ya bajeti yake katika masuala ya tafiti ambapo
wataalamu wa Tafiti hizo ambao ni Wanasayansi watatakiwa kuwa wabunifu
na kufanya tafiti mbalimbali katika maeneo ya Viwanda  hali ambayo
itachangia sana kuendeleza maendeleo ya  Nchi ya Tanzania.

Katika hatua nyingine  Makamu mkuu wa chuo hicho Profesa Burton
Mwamila alisema kuwa, chuo hicho kitakuwa  na faida kwa jamii hali
ambayo itaweza kupunguza na kuondoa matatizo mbalimbali hasa kwenye
fani za sayansi ,uandisi na teknolojia kwa ajili ya maendeleo ya taifa
na kuweza kupata wataalamun wenye uwezo na ujuzi  wa kutosha .

‘Tunategemea mabadiliko makubwa sana hasa kwa nchi ya Tanzania kwani
chuo hiki kina uwezo mkubwa sana wa kuwapa fursa watanzania kuwa na
ujuzi wa kutosha hasa katika maswala ya tafiti na sayansi na kama
watanzania wataweza kukitumia vyema ni wazi kuwa fursa nyingi
zitaongezeka sana’alisema Profesa Mwamila.

Alisema kuwa, ili kujua kuwa chuo hicho kina nafasi kubwa sana kwa
watanzania chuo hicho kimeamua kudahili jumla ya wanafunzi 83 huku
wanafunzi 30 wanachukua masomo ya uzamivu na 53 ni mafunzo ya uzamili
ambapo kama wote hao watamaliza masomo ya vyema basi wataweza
kuchangia kuongezeka kwa pato la taifa na hatimaye uchumi wan chi
kukua.

Mwamila alisema kuwa, katika mwaka huu wa masomo chuo kimedahilin
wanafunzi 135 wa kundi la pili, huku kati yao 46 wanachukua masomo ya
uzamivu na 89 watachukua masomo ya uzamili huku asilimia 22 ni
wanawake , ambapo chuo hicho kwa sasa kina jumla ya wataalamu
watarajiwa 217 kati yao asilimia 20 ni wanawake.

‘Ili kujua kuwa masomo ya sayansi ni muhimu kwa wanawake tumehakikisha
kuwa idadi ya wanawake inakuwa kwa kasi tofauti na vyuo vingine nah ii
itasaidia kufanya taaluma ya sayansi kuwa na wataalamu wengi ambao ni
wanawake tofauti na ilivyo hivi sasa kuwa wenye taaluma wengi ni
wanaume,ingawaje kuna fursa kama ya chuo hicho lakini haitumiwi
ipasavyo ‘alisema Mwamila.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates