kamera yetu ilifanikiwa kupiga picha wataalam hao wakikusanya vifaa vyao kurudi makwao baada ya kuuza dawa za kutosha |
moja ya TV iliyokuwa ikishindaniwa ikiwa juu ya meza wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo wakikusanya kilicho chao baada ya kuahirisha zoezi hilo bila taarifa kwa wateja wao |
kampuni ya dawa ya mswaki aina ya Colgate yadaiwa kutapeli wakazi wa jiji la mapena jana eneo la shoprite baada ya kuja kwa mtindo wa mchezo wa bahati nasibu na kuwataka wananchi kununua dawa hiyo ya Colgate mbili yenye gharama za shilingi 5000 kwa mbili kwa kigezo cha kuingia kwenye droo ya kushinda TV.
Watu hao waliokuwa wakiwaita watu
kwa kucheza mziki na kuwasisitiza watu kununua dawa ili kuweza kuingia
kwenye droo ya mchezo huo kwa kupewa fom maalum ya kujaza ambapo baadae
kwa hali isiyo ya kawaida waliamua kuhairisha na kuondoka eneo la tukio
kimya kimya hali iliyozua tafrani baina ya watu waliokuwa wakisubiri
droo hiyo kuchezeshwa.
Mzee mmoja aliyejimbulisha kwa jina moja la Amiri alisema kuwa majira ya saa sita mchana alikwenda eneo la SHOPRITE kwa ajili ya kununua mahitaji ya nyumbani kwake ndipo alipokutana na watu hao wa kampuni ya Colgate na kumlazimisha kununua dawa ili kuingia kwenye droo ya kushinda Televission ya bapa screen.
Hata hivyo aliendelea kulalama
mbele ya waandishi wa habari kuwa baada wa watu wengi kununua dawa hizo
za mswaki na kutoona matokeo ya mchezo huo kuchezwa ndipo walipoenda
kuuliza na kuambiwa mchezeshaji bahati hajafika hivyo waendelee kusubiri
ambapo baadhi walikata tamaa na kuondoka giza lilipoanza kuingia.
"Hata hivyo baadae majira ya saa
12 jioni tulichoka kusubiri ndipo kuamua kuongea kero zetu kwenu kwani
hawa jamaa wametutapeli kwa kutudanganya tununue dawa kwa madai kuna
droo ya kushindania VT, Ndio tukaulizana kama sokoni kumedorora kwanini
watudanganye si watoe tu matangazo kwenye vyombo vya habari" alisema
mzee huyo.
Mwandishi wa habari hizi alifika
eneo la tukio eneo la SHOPRITE na kukutana na wafanyakazi hao ambao
hawakutaka kutaja majina yao wakikusanya vifaa vyao huku lundo za kuponi
zilizojazwa kuashiria wameuza dawa za kutosha zikionekana kupangwa.
Aidha waandishi wa habari hizi
walifika eneo la tukio na kukutana na wafanyakazi wa kampuni hiyo
wakikusanya vifaa vyao ikiwemo kuondoa maturubali yao pamoja na TV kwa
madai kuwa walipanga kweli kufanya shindano lakini mtaalamu wa bahati
nasibu hajatokea