Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiongoza harambe ya kuchangia ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike katika Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji, kinachomilikiwa na Kanisa la Moravian nchini Tanzania,Jimbo la Kusini Magharibi,usharika wa Ruanda mjini Mbeya.Katika Harambee hiyo,Mh. Lowassa pamoja na marafiki zake wakiweza kuchangia sh millioni 25 kusaidia ujenzi huo.
Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiendesha harambe ya kuchangia ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike katika Chuo Kikuu cha
Teofilo Kisanji, kinachomilikiwa na Kanisa la Moravian nchini
Tanzania,Jimbo la Kusini Magharibi,usharika wa Ruanda mjini Mbeya.Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Rungwe,Mh. Cripin Meela.
Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimuhamasisha mmoja wa waalikwa kuchangia katika harambe ya kuchangia ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike katika Chuo Kikuu cha
Teofilo Kisanji, kinachomilikiwa na Kanisa la Moravian nchini
Tanzania,Jimbo la Kusini Magharibi,usharika wa Ruanda mjini Mbeya.
Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (wa pili kushoto) akifurahia jambo wakati alipokuwa katika Mazungumzo na Askofu Kiongozi wa Kanisa la Moravian Tanzania (KMT), Askofu Alinikisa Cheyo (kushoto) wakati wa hafla ya harambe ya kuchangia ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike katika Chuo Kikuu cha
Teofilo Kisanji, kinachomilikiwa na Kanisa la Moravian nchini
Tanzania,Jimbo la Kusini Magharibi,usharika wa Ruanda mjini Mbeya..
Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiagana na viongozi mbalimbali wa Chuo hicho mara baada ya kuongoza harambe ya kuchangia ujenzi wa bweni la wanafunzi wa kike katika Chuo Kikuu cha
Teofilo Kisanji, kinachomilikiwa na Kanisa la Moravian nchini
Tanzania,Jimbo la Kusini Magharibi,usharika wa Ruanda mjini Mbeya.
WAZIRI Mkuu Mstaafu Edward Lowassa amewataka vijana nchini
kusoma kwa bidii ili kutoa ushindani katika soko la jira la Afrika Mashariki
(EAC).
Lowassa aliyasema hayo jana jijini Mbeya alipoongoza
harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa mabweni ya Wasichana Chuo Kikuu cha
Teofilo Kisanji kinachomilikiwa na Kanisa la Moravani Tanzania.
Katika harambee hiyo Lowassa, familia na marafiki zake
walichangia fedha taslimu Sh. Milioni 20, ahadi Sh. Milioni 5 na kufanya jumla alizochangia
kuwa Sh. Milioni 25.
Akizungumza katika harambee hiyo alisema, unyonge wa
wasichana wa kike mashuleni hauwezi kuondolewa kwa kelele za kisiasa hata siku
moja.
“Unyonge wao hauwezi kuondoka kwa kelele za kiasiasa tu,
bali ukombozi wao kwa sehemu kubwa upo mikononi mwao kwa maana ya elimu,”
alisema Lowassa.
Alisema hivi sasa taifa la Tanzania limekuwa na idadi kubwa
ya vijana ambao kwa namna yoyote wanapaswa kuandaliwa vizuri.
“Katika taifa letu vijana ndio wengi zaidi hivyo ni muhimu tuwaandae
vizuri endapo tunataka kuwa na taifa madubuti,” alisema Lowassa na kuongeza:
“Mwalimu Nyerere alitufundisha; kupanga ni kuchagua. Hivyo
natoa mwito kwa wasichana mjiepushe na viwashiwi na msome kwa bidii,”alisema.
Akifafanua kuhusu umuhimu wa ujenzi wa Hosteli za wasichana
mashuleni na vyuoni unatokana na wasichana wengi kukabiliwa na mazingira magumu
yanayotishia mustakabli wa maisha yao.
Alisema kwa sasa Jumuiya ya Afrika Mashariki tayari imefungua
mipaka yake ya ajira huria hivyo kama vijana nchini wataendelea kukosa elimu
basi ushindani katika soko hilo utakuwa mgumu.
“Ndugu zangu nawaomba tuunganishe nguvu tuwasaidie vijana
wetu, naamini tukitoa Mungu hata acha kutubariki na atabariki kazi zetu
kuongeza riziki zetu.
“Rafiki zangu wadai mimi ni tajiri nina fedha nyingi, si
kweli ninafanya jambo hili kwa kushirikisha rafiki, ndugu na jamaa zangu tangu
nianze kutoa sijafirisika,” alisema Lowassa.
Awali Askofu Kiongozi wa Kanisa la Moravian Tanzania
Alinikisa Cheyo akizungumza katika harambee hiyo alisema, kukamilika kwa
mabweni hayo kutasaidia wasichana 348 kukaa sehemu moja kwenye vyumba 87.
“Tumejipanga kukusanya Sh.Milioni 235 katika harambee hii,”
alisema Askofu Kiongozi Cheyo.
Naye Mkuu wa wilaya ya Rugwe Chrispn Meela akizungumza kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abass Kandoro alisema, serikali itaendelea kuwa
karibu katika kuhakikisha mabweni hayo yanakamilika.
“Serikali inaendelea kuunga mkono juhudi hizi kwani ni
lazima tuwekeze katika elimu na kwa kutambua hilo tunatoa Sh. Milioni Moja,”
alisema Meela.