Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya
Longido limesema kuwa halitakubaliana na mwekezaji wa kujenga kiwanda cha
Magadi kujengwa katika wilaya ya Monduli na Malighafi hiyo kuchukuliwa katika
wilaya ya Longido.
Akizungumza
katika baraza la madiwani lililofanyika katika wilaya hiyo makamu mwenyekiti wa
halmashauri hiyo Esupat Ngulupa alisema kuwa haiwezekani mali ghafi zote
zipatikane katika wilaya ya longido alafu mwekezaji akajenge kiwanda katika
wilaya nyingine.
Esupat
alisema kuwa ni lazima madiwani waoneshe msimamo katika kujali maslahi ya wananchi wa longido kwa umuhimu
mkubwa sana kwa kuwa mchakato huo tangu mwanzo ulikuwa unaonesha kuwa kiwanda
cha uvunaji wa magadi yaani (SODA ASH MINING) kitajengwa katika wilaya tayarimadiwani walishaanza mchakato wa
kufuatilia kwa karibu mpango huo ikiwa ni pamoja na kufanya ziara nchini Kenya.
“Nataka
niwahakikishie kuwa hatutakubali kiwanda kijengwe Wilaya ya Monduli
wakati magadi hayo yanapatikana ziwa natron ambalo lipo hapa kwetu hatutakubali
mana tunajua wazi kuwa mwekezaji atakuwa amepewa taarifa tofauti kwa hili
hatutakubali kabisa longido inajitegemea na monduli vivyo hivyo.”alisema Esupat
Aliongeza kuwa
Rasilimali hiyo ni muhimu sana hivyo ni lazima kiwanda hicho kijengwe wilayani
longido ili kiwanufaishe wakazi wa eneo hilo kutokana na vitendea kazi ambavyo
vinapatikana wilayani hapo.
Kwa upande
wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo Joseph Ole Sadira alisema kuwa madiwani wa
halmashauri hiyo wanaunga mkono kwa asilimia mia moja mwekezaji huyo kujenga
kiwanda hicho katika wilaya ya longido ili kiweze kuwanufaisha wananchi wa eneo
hilo.
Pia alisema
kuwa tayari madiwani walishafanya ziara nchini Kenya ili kujionea jinsi wanavyofanya
kazi hiyo na mafanikio ambayo wameyapata
kutokana na uvunaji wa magadi hiyo na amebainisha kuwa magadi yaliyopo
wilayani hapo ni bora kuliko yanayopatikana Kenya.
Sadira
alisema kuwa tayari Wilaya hiyo ilishaufuatilia uwekezaji huo kwa kina na zaidi
na kuingia hata nchi jirani na kuchunguza faida za uvunaji huo katika kiwanda
kilichopo nchini Kenya
Alisema kuwa
kutokana na utafiti uliofanywa ulibainsha faida kubwa sana itapatikana kama
watajiingiza katika mradi huo hivyo hawatakubaliana na mwekezaji kuchukua
malighafi hiyo na kunufaisha wananchi wa wilaya nyingine ili hali waliopo hapo
hawanufaiki na chochote.
Naye mkurugenzi
mtendaji Julius Chalya alikiri kuwa
tayarimadiwani walishafanya ziara katika nchi jirani kama Kenya na kujionea
mafanikio waliyoyapa kutokana na uwekezaji huo hivyo kuwepo kwa kiwanda hicho
katika wilaya ya longido kutaleta tija sana na maendeleo kwa wilaya hiyo ambayo kwa kiasi
kikubwa wananchi wake ni jamii ya Wafugaji.