LIGI ya
Moivaro imeendelea kutimua vumbi katika viwanja mbalimbali jijini Arusha ambapo
hivi karibuni mechi tano zimechezwa kwa nyakati tofauti huku klabu za Future
Stars ikionekana kung”ara katika ligi hiyo.
Ligi hiyo
ilizinduliwa mwezi Septemba mwaka huu na kocha wa Stars nchini,Jan Poulsen kwa lengo la kukuza soka
la vijana nchini sanjari na kuibua vipaji mbalimbali vya soka.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa na katibu wa ligi hiyo,Alfred Itaeli alisema kwamba katika
uwanja wa St,Constantine timu ya Future Stars upande wa wanawake U 17 iliichapa
Orkeeswa mabao 4_0 huku ile ya wavulana ya
U 17 ikiichapa timu ya Orkeeswa mabao 2_1.
Katika
uwanja wa Ngaramtoni timu ya Habari Maalum ilijikuta ikiambilia kipigo cha
mabao 6_0 kutoka kwa klabu ya Chipukizi na katika uwanja wa shule ya kimataifa
ya Moshi timu ya Mambas iliichapa timu ya Future Stars kwa jumla ya mabao 4_1
huku mechi ya mwisho katika uwanja wa TGT
klabu ya Orkeeswa iliichapa St Constantine kwa mabao 2_1.