Mgeni Rasmi katika Onyesho la Khanga za Kale,Waziri wa Maendeleo
ya Jamii,Jisnia na Watoto,Mh, Sophia Simba akisoma hotuba yake fupi
wakati wa kufungua rasmi Onyesho la Mavazi ya Khanga za Kale
linaloratibiwa na Mamaa wa Mitindo,Asia Idarous Khamsin (kushoto) chini
ya Kampuni yake ya Fabak Fashion.Onyesho hilo limefanyika usiku huu
katika Hoteli ya Serena,Jijini Dar es Salaam.
Muandaaji wa Onyesho la Mavazi ya Khanga za Kale,Mamaa wa
Mitindo,Asia Idarous Khamsin akizungumza machache kabla ya kuanza Rasmi
kwa Onyesho hilo lililofanyika usiku huu katika Hoteli ya Serena,Jijini
Dar es Salaam.
Washiriki wa Shindano la Unique Model,wakiwa Jukwaani wakati wakipita kuonyesha vazi hilo la Khanga za Kale.
Baadhi ya Wanamitindo wakipita Jukwaani kuonyesha mavazi ya aina
Mbali mbali yaliyobuniwa na Wabaunifu zaidi ya 30 walioshiriki kuonyesha
mavazi yao katika Onyesho hilo.
Mzee Khamsin na Mama Asia Idarous Khamsin wakipita jukwaani kutoa shukrani.
Mtaalam wa Vazi la Ghanga akitoa Somo.
Pongezii....
Wageni wa aina mbali mbali na kutoa sehemu mbali mbali pia walikuwepo kwenye Onyesho hilo.
Ilifika wakati wa Kutoa Tuzo za Shukrani,ambapo Mama Ankal (kulia) alipokea Tuzo ya Globu ya Jamii.
Mkurugenzi wa Prime Time,Juhayna Kussaga akipokea Tuzo kwa niaba ya Clouds TV.
Mwanalibeneke Othman Michuzi wa Libeneke la MTAA KWA MTAA
BLOG,akipokea Tuzo ya Blog yake kwa Mchango mkubwa aliounyesha juu ya
Shindano hilo.
Ankal Issa Michuzi akipokea Tuzo kwa niaba ya Blog ya Jiachie ambayo ipo chini ya Michuzi Jr.
Misie Popular pia alilamba nondozz yake.