Ndugu mwenyekiti wa Hai Teachers Saccos,
Ndugu wajumbe wa bodi ya chama,
Ndugu katibu mkuu wa Hai teachers Saccos,
Ndugu maofisa ushirika wa wilaya za Hai na Siha,
Ndugu mkaguzi wa coasco,
Ndugu meneja wa chama,
Ndugu wajumbe wa mkutano mkuu
Ndugu wageni waalikwa
Mabibi na mbwana,
Asalaam aleikhum,bwana yesu aifiwe,tumsifu yesu kristu
Ndugu mwenyekiti,awali ya yote nimshukuru mwenyezi mungu kwa kuweza kutukutanisha leo katika mkutano huu mkuu wa kawaida unaolenga kuboresha hali yetu ya maisha na kutuletea hali ya ustawi.
Lakini pili kukushukuru wewe pamoja na kamati yako nzima ya usimamizi kwa kunipa heshima kubwa ya kuwafungulia mkutano wenu mkubwa ambao pia ni fursa nzuri ya kukutana nanyi mkiwa kama kundi kubwa katika jamii yetu hapa Hai.
Ndugu mwenyekiti na wajumbe wa mkutano huu nianze kwa kuwapongezeni sana kwa kuweza kudumu kwa miaka kumi na mitano tangu kuanzisha chama chenu cha akiba na mikopo mnamo Julai mosi,1993 .
Ni hatua muhimu na mafanikio makubwa sana kuweza kuhimili changamoto mbalimbali hadi kufikia umri huo huku mkiwa na idadi ya wanachama 717 wengi wao wakiwa akinamama lakini kikubwa mkimiliki ofisi yenu wenyewe na si ya kupanga.
Ndugu mwenyekiti,Ushirika ndiyo mkombozi na nguzo kuu ya mwananchi wa kawaida akiwemo mtumishi wa serikali hata wa sekta binafsi katika kumkomboa kiuchumi na hili lipo wazi na inajidhihirisha kutokana na historia ya nchi yetu hadi kufikia kuanzishwa kwa hivi vyama vya ushirika wa mikopo na akiba.
Kihiistoria shughuli za ushirika zilianza miaka kabla ya uhuru wa nchi yetu na kuendelezwa baada ya uhuru kwa kuwemo katika utekelezaji wa sera na mipango iliyotelelezwa na serikali kati ya mwaka 1961 na 1966 kwa kugawanywa kwa vipindi viwili vya miaka mitatu mitatu.
Chanzo cha kuanzishwa kwa ushirika kilitokana na matokeo ya sera na mipango hiyo ya serikali kwa kimwangalia zaidi mkulima masikini ambapo katika kilimo utekelezaji wa mipango hiyo ulikuwa na mafanikio katika ununuzi wa mazao ya mkulima.Uwezo wa kununua mazao uliongezeka.Aidha suala la mkulima kuwa na taasisi inayomtetea lilijitokeza na kuungwa mkono.Vyama vya ushirika viliimarishwa na ilipofika mwaka 1966,tayari kulikuwa na vyama vya ushirika 33 na vyama vya msingi 1,500
Kimsingi historia hii inaonyesha jinsi vyama vya ushirika vilipoanzishwa vilikuwa njia dhahiri ya kumuendeleza mkulima mdogo na kumlinda dhidi ya unyonyaji wa wafanyabiashara na wachuuzi.
Katika kipindi hicho vyama vya ushirika vilifanya vizuri na vilikuwa vimejiimarisha katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii.vilimiliki mali na kuwa na mitaji mikubwa ya kuendesha shughuli zao.Mali hizo ni pamoja na ardhi,majengo makubwa ya ofisi,mashamba makubwa,viwanda vya kuchambua pamba na katani,viwanda vya kukoboa kahawa na mpunga,viwanda vya kukamua mafuta,magari,matrekta na maghala.
Ndugu mwenyekiti,Sasa ukija kwa upande wa vyama vyetu hivi vya ushirika vya akiba na mikopo(saccos) ni asasi za fedha zinazoundwa na watu waliojiunga pamoja kwa hiari yao ambao wamekubaliana kuweka fedha zao kwa pamoja na kukopeshana kwa lengo la kujiendeleza kiuchumi na kijamii.
Msisitizo mkubwa hapo kwa wanachama ni kujijengea tabia ya kuweka akiba na suala la mkopo huja baadaye kulingana na mahitaji na hivyo mwanachama anatakiwa kukopa kwa busara na kulipa kwa wakati.
Kwa upande wa nyinyi wanachama wenye umri mkubwa kidogo mtakumbuka kwamba baada ya azimio la arusha,mipango na shughuli za kiuchumi na maendeleo ya yalibadilika kwa kiwango kikubwa.Serikali ilianzisha benki maalumu kwa ajili ya shughuli za kiuchumi.
Mathalani ili kuwasaidia wakulima na vyama vya ushirika serikali ilianzisha benki ya taifa ya ushirika mwaka 1964.Katika kurahisisha upatikanaji wa rasilimali fedha katika shughuli nyingine,benki ya taifa ya biashara ilianzishwa mwaka 1965.Serikali ilimiliki asilimia sitini ya hisa katika benki hiyo.
Kufuatia kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi pamoja na upungufu uliokuwepo katika bodi ya pamoja ya sarafu ya Afrika ya Mashariki(East Africa Currency Board),mwaka 1966 serikali ilianzisha benki kuu ya Tanzania kwa lengo la kuiwezesha serikali kusimamia upatikanaji na usambazaji wa huduma za kifedha katika sekta mbalimbali za kiuchumi na kusimamia shughuli mbalimbali za benki nchini.
Katika kipindi hicho,Benki kuu ya Tanzania ilianza kutoa sarafa ya Tanzania Bara.Serikali iliongeza nyumba bora na majengo ya kisasa kwa kuanzisha Benki maalumu ya nyumba mwaka 1995.
Hata hivyo bado eneo hili lilikabiliwa na changamoto nyingi kama ilivyo kwa maeneo mengine.Mapato ya serikali,kwa kiwango kikubwa yaliendana na maendeleo yaliyopatikana kwenye sekta nyingine.Vyanzo vya mapato yatokanayo na kodi mbalimbali havipanuki sana.Ushuru wa forodha na kodi ya mauzo zilichangia mapato ya serikali kwa kiwango kikubwa.Kodi itokanayo na ajira ilikuwa kidogo kwa sababu sehemu kubwa ya wananchi waliajiriwa katika kilimo.Udogo wa sekta ya viwanda na sekta binafsi na ukubwa wa sekta iliyoko nje ya mfumo wa fedha ni baadhi ya mambo yaliyosababisha mapato ya srtikali kuwa madogo.
Ndugu mwenyekiti sasa ukiangalia mtiririko huo kwa miaka mingi sana watumishi kwa maana waajiriwa walijitenga na mfumo huo wengi kutegemea zaidi kuishi kwa mshahara huku hali ya maisha ikiendelea kubadilika kutokana na mabadiliko mbalimbali yanayotokea duniani.
Uwezekano wa kupata mikopo katika mabenki ulikuwa mdogo kutokana na masharti na lililokubwa ni lile la dhamana kwa mkopaji.
Ndipo ikaonekana njia pekee ya kumkomboa mtumishi wa umma kiuchumi ni kwa yeye na wenzake kujiunga pamoja na kuanzisha vyama hivi kwa ushirika kwa kukusanya pamoja fedha zao na kukopeshana.
Ndugu mwenyekiti,mfumo huo ulikubalika na kubarikisa na serikali kwa kuwa ulionekana ndiyo njia rahisi zaidi ya kuboresha hali ya watumishi na kuwawezesha kutimiza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa zaidi.
Kuanzia hapo kumekuwepo na mipango mbalimbali ya kuhakikisha kwamba serikali inashiriki kikamilifu katika kuhakikisha hivi vyama vinaimarika na kuwa kweli mkombozi wa mwananchi katika kujijenga kiuchumi na kijamii.
Ndugu mwenyekiti mikakati ipo mingi mfano Katika utekelezaji wa malengo ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania(MKUKUTA) na ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005-2010,serikali wilayani Hai kupitia idara ya ushirika imeyekeleza mambo mbalimali yakiwemo ;
1.Kutoa mafunzo kwa bodi za vyama vya ushirika kuhusu majukumu yao ya kila siku
2. Kuhamasisha wananchi kujiunga na vyama vya ushirika
3. Kuhamasisha wananchi kuanzisha vyama vya akiba na mikopo SACCOS.
3. Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara katika vyama vya ushirika.
4. Kutoa mafunzo kwa wanachama kuhusu haki na wajibu wao.
5. Kuimarisha kuendeleza vita dhidi ya rushwa katika vyama vya ushirika
Tayari katika wilaya ya Hai tuna zaidi ya vyama vya ushirika 68 vya aina mbalimbali kama ifuatavyo ;
-Vyama vya mazao hususani kahawa 25.
-Vyama vya akiba na mikopo SACCOS 30.
-Vyama vya maziwa 7
-Vyama vya umwagiliaji 2
-Vyama vya ushirika vya uzalishaji biashara 2
-Vyama vya ushirika vya uzalishaji asali 1
Kuongezeka kwa idadi ya vyama vya ushirika na mikopo kumesaidia kuongeza idadi ya wanachama kwani hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2010/2011 wanachama 2,859 waliongezeka kutoka wanachama 25,024 hadi kufikia wanachama 27,859,kuongezeka kwa vyama vya akiba na mikopo (SACCOS) kutoka 20 hadi 30,wanachama waliongeza hisa na kufikia shilingi 366,566,939,kuongeza akiba na kufikia shilingi 1,145,011,320 na amana kufikia shilingi 385,659,298 hivyo hata mikopo inayotolewa kwa wanachama imekuwa na wigo mpana kwa kufikia shilingi 3,711,037,374.
Vyama vingi vya akiba na mikopo vijijini wanatumia teknolojia ya kompyuta katika kutunza mahesabu ya fedha za wanachama.Hadi sasa kuna vyama vinnne ambavyo vinatumia teknolojia hii huku saccos mbili zikianzisha mpango wa stakabadhi ghalani kwa mazao ya nafaka.
Ndugu mwenyekiti,Walimu ni vyema kutumia chama chenu hiki cha kuweka na kukopa kupata mitaji ya kufanyia shughuli mbalimbali badala ya kwenda moja kwa moja mtu binafsi katika taasisi za fedha na kujikuta ana madeni mengi ambapo kimsingi yanawafanya kukosa ari ya kufundisha na kurudisha nyuma ufaulu wa wanafunzi.
Tayari kuna taarifa kwamba kuna walimu wanakabiliwa na madeni mengi yanayotokana na mikopo wanayochukuwa katika taasisi mbalimbali za fedha baadhi ya taasisi ni zile ambao zinaota kama uyoga huku zikiwa na riba kubwa sana.
Madeni hayo makubwa ya mikopo kwa baadhi ya walimu kutoka katika taasisi mbalimbali za fedha yanachangia kuzorotesha utendaji wenu wa kazi na kushindwa kufundisha kwa ufasaha madarasani.
Kwani badala ya kufanya kazi zenu kwa ufasaha,wamekuwa wakitumia muda mrefu kwenda kusaka fedha za marejesho na pia kujiweza kuishi
Aidha ni vyema nyinyi walimu wa hapa Hai kuamua kukopa fedha kwa malengo hasa ya kujikwamua kiuchumi na siyo kukopa bila ya kuwa na malengo ya kimaendeleo
Mmezungumzi uwezo mdogo wa kukopeshana na riba kubwa ya mabenki ni vyema katika kukabiliana na hali hiyo mkaanza mkakati wa kuwashawishi wanachama wenu kuunua hisa zaidi ili kukiongezea mtaji chama chenu kwa lengo la kuondokana na mfumo wa sasa wa kutegemea mikopo ya taasisi za fedha ambayo tayari mmedai yanatoza riba kubwa.
Ni vyema mkaanza sasa kuwashawishi wanachama wenu umuhimu wa kununua hisa ambao endapo zitaongezeka mtakuwa na mtaji wa kutosha wa kukopeshana,
Hivi sasa natambua na nyinyi wenyewe mnalifaha hilo kwamba mna egemea zaidi mikopo kutoka taasisi za fedha na hivyo kukuta mna bakiwa na faida ndogo sana kutokana na riba kubwa sana za taasisi hizo za fedha
Aidha ni vyema pia mkaandaa mpango mkakati na andiko kwa ajili ya mradi ili chama kiwe na njia mbadala nyingi za kukiongeze mtaji.
Ndugu mwenyekiti nimefarijika kusikia katika risala yenu katika miongoni mwa malengo ni pamoja na kuwekeza kwenye makampuni na taasisi za kifedha nafahamu kuwa ni pamoja na kununua hisa na kufungua akaunti maalumu kwa muda maalumu.
Lakini pia kujenga ukumbi wa mikutano na hapa naongeza kuwa wa kisasa kwani mji wetu huu hivi sasa unakuwa kwa kasi na hauna ukumbi wa mikutano lakini lingine ni hosteli na shule za awali.
Kadhalika mmezungu,zia kuwa na vyombo vya mawasiliano kama simu,internet,fax na mpesa,ni wazo zuri kwani ni huduma ambazo zina watumiaji wengi na kwa upande wenu tayari mnasoko kwani kwa kuanza wateja wakubwa ni nyinyi wenyewe walimu.
Ndugu mwrnyekiti ,Tofauti na saccos nyingine za taasisi mbalimbali,nyinyi walimu mnanafasi kubwa ya kufika mbali kutokana na asili ya ajira zenu ambazo mara nyingi umwezesha mwajiriwa kuwemo katika ajira kwa muda mrefu mpaka pale atakapostafu ajira kwa mujibu wa sheria.
Ndugu mwenyekiti mfano wa hili nalozungumzia wengi mtakuwa mnaukumbuka kwamba miongoni mwa vyama vya akiba na mikopo vilivyokuea na nguvu sana ni pamoja na iliyokuwa inaundwa na shirika la posta na simu wakati yakiwa shirika moja lakini lilipotokea zoezi la upunguzaji wa watumisha hasa kwa shirika la simu lilihatarisha sana idadi ya wanachama
Kwa hiyo ni vyema mkajibunia mfumo huo uliopo na kuutumia kuhakikisha kwamba mnaimarisha chama chenu na kuwa wabunifu wa kuhakikisha mnatumia kila fursa kikiimarisha na hatimaye kuwa mkombozi wa kweli wa mwanachama.
Ndugu mwenyekiti kuna chamgamoto mbalimbali ambazo umezitaja lakini kubwa na za awali ni kwa kucheleweshwa kwa makato ya wanachama kutoka katika halmashauri ya wilaya za Hai na Siha pamoja na orodha ya wakopaji kutoingizwa katika kompyuta kwa wakati na hivyo kukosesha chama mapato.
Kwa upande wa wilaya ya Hai,changamo hiyo ni ya kweli kabisa kwani kwa miezi mitatu mfululizo iliyopita kumekuwepo na kuchelewa kwa makato hayo mfano hundi ya mwezi Septemba iliingia Oktoba 18,hundi ya oktoba iliingia Novemba 22 na hundi ya Novemba iliingia tarehe 11 ya mwezi huu.
Changamoto hiyo ni ya utendaji zaidi na ndiyo kwanza nimeipata hivyo ni ya kiutendaji zaidi hivyo nitahakikisha naisimamia ili kurekebisha hali hiyo na kwa upande wa Siha kwa kuwa ni wailaya ya jirani basi ujumbe huu nitaufikisha katika mamlaka sinazohusika.
Ndugu mwenyekiti,suala la changamoto la mtaji mdogo nimelizungumzia ambapo kwa kurudia ni kuhakikisha sasa mnaonbeza idadi ya wanachama na pia kuwahamasisha waliopo kununua hisa na kuongeza akiba na kwa upande wa wanachama wanaokopa katika taasisi nyingi za fedha kwa wakati mmoja kama nilivyosema hapo awali limekuwa kero kubwa sana.
Ndugu mwenyekiti kinachohitajika hapo ni elimu kwa wanachama wetu lakini pia kuwa karibu zaidi na taasisi zinazopitisha mikopo hiyo kwa kuhakikisha taratibu zinafuatwa kabla ya kuidhinishwa kwa mikopo.
Ndugu mwenyekiti na ndugu wajumbe,kama nilivoanza,kabla ya kumaliza,naomba niwashukuru tena kwa kunialika katika mkutano wenu huu mkuu kwani nimweza kupata fursa nzuri ya kuweza kuongea nanyi
Asanteni kwa kunisikiliza