Chama
cha mchezo wa baiskeli Taifa (CHABATA) kinatarajia kupeleka wachezaji
10 nchini Afrika kusini kuwakilisha nchi kwenye mashindano ya kusaka
bingwa wa bara la Afrika yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi February
tisa hadi 14 mwaka huu.
Akizungumza
na libeneke la kaskazinihili mwenyekiti wa Chama cha mchezo huo nchini Godfrey Jax
Mhagama amesema kuwa mashindano hayo yanayoshirikisha nchi zaidi ya 30
za bara la Afrika yanafanyika kila mwaka ambapo kwa Tanzania wachezaji
hawa watakuwa wanaifanya nchi kuwa mara ya tano kushiriki.
Mhagama
alisema kuwa wachezaji hao wanatarajia kuondoka nchini February sita
mwaka huu kulingana na upatikanaji wa fedha wa dola 12,000 (milioni 20)
ambapo amesema kuwa kwa sasa chama hicho kina nusu ya fedha hizo.
“Kwa
mwaka huu tunatarajia kupeleka wachezaji 10 miongni mwao wasichana
wakiwa ni wawili na wanaume nane, lakini hilo litafanikiwa endapo
wadhamini watajitokeza kutusaidia kupunguza gharama kwani hadi sasa tuna
dola 6000 na bajeti yetu kwa hao watu 10 ni dola 12,000 hivyo kama
tukikosa itabidi tuangalie namna ya kupunguza idadi” alisema mhagama.
“Kwa
sasa nitumie fursa hii ya chombo chenu kinachosomwa na watu wengi
nchini kuliko vyombo vyovyote kuwaomba wadau wajitokeze kusaidia timu
hii ikafanye vema huko Afrika kusini kwani endapo tukifanikiwa kupeleka
wachezaji wengi zaidi ndio tutakuwa katika nafasi nzuri ya kushinda
lakini watu wachache huwa rahisi kuachwa”
Miongoni
mwa wachezaji hao wane wanaotoka mkoani Arusha akiwemo msichana mmoja
imebainika kuwa bado hawajaingia kambini hadi leo ambapo kila mmoja
anafanya mazoezi mkoani kwake huku vifaa vyao ikiwemo baiskeli kutokuwa
na uimara wa mashindano.
Akijibu
swala hilo Mhagama alisema kuwa ni kweli hadi leo wachezaji hawajaingia
kambini kufanya mazoezi kutokana na kutokuwa na fedha za kugharamia
mahitaji yao hali iliyosababishwa na ukosefu wa ufadhili kwa kupatiwa
ahadi na makampuni mbalimbali zisizotekelezeka.
“Ni
kweli kama ulivyowaona hawajaingia kambini kutokana na kukosa fedha za
kugharamia kambi, huku wadau wakituahidi tu bila kutekeleza lakini
naomba niwahakikishie wadau kuwa hilo pamoja na kuwa kama sehem ya
madhara kwetu lakini wasiwe na wasiwasi kwani tutajitahidi kuwa katika
nafasi nzuri”