Katika
picha ni Noel Olevaroya akihutubia Maelfu ya wananchi katika moja ya
harakati zake katika mkutano wa chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA)
********
Aliyewahi
kuwa mwenyekiti wa vijana na mjumbe Wilaya ya Arusha kupitia chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Noel Olevaroya (37) ametangaza rasmi
kupeperusha bendera ya chama hicho kwa kuwania nafasi ya ubunge katika
jimbo la Arusha mjini
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha Noel Olevaroya
alisema kuwa nia yake ya kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la
Arusha ni msukumumo kutoka kwa Mungu baada ya kumaliza nafasi yake ya
uwenyekiti wa vijana na mjumbe wilaya ya Arusha mwaka 2014
Alieleza
kuwa msukumo huo ulikuwa ukimsumbua sana na ndipo aliamua kutii sauti
ya Mungu kwa kutangaza kuwania nafasi hiyo ya kugombea kiti cha ubunge
katika jimbo la Arusha mjini ambapo kwasasa jimbo hilo lipo mikononi mwa
Godbless Lema
Aidha
alisema kuwa Mbunge anafursa nzuri sana ya kusaidia wananchi hata kwa
kupitia mfuko wa jimbo,mshahara hali ambayo itasaidia kuwainua wananchi
na kupunguza umaskini
Alitoa
wito kwa vijana wa Arusha kusikiliza sauti ya Mungu kwa kuwachagua
viongozi bora wenye hofu ya Mungu kwa maslahi ya Nchi yetu