Photo: http://www.photos.apo-opa.com/index.php?level=picture&id=1763
Wa Kusambaza Umeme Afrika Mashariki
NAIROBI, Kenya, February 18, 2015/ -- Tunavyoshuhudia
viwanda katika bara hili viking'ang'ana kutengeneza na kusambaza umeme
unaotosha kufikia kiwango msingi, usambazaji unaonekana kuwa changamoto
kubwa zaidi kwa ufikiaji wa umeme barani Afrika.
Kwa
sasa, kuna viwango vya uwekezaji ambavyo havijawahi kuonekana katika
sekta ya uzalishaji umeme- haikaribii tu utafutaji tena. Wawekezaji leo
wanaona uzalishaji umeme kama fursa iliyotajwa na watu wengine kuwa
kubwa kiasi kwamba itafanya mapato ya makampuni makubwa ya simu barani
Afrika yaonekane kuwa madogo.
Hata
hivyo, licha ya zaidi ya dola bilioni 8 za Marekani kuwekezwa katika
miradi mipya nchini Afrika Kusini peke yake, usambazaji unaendelea
kuporomoka, huku ukiathiri hali ya kijamii na siasa katika bara la
Afrika pakubwa. Zaid ya hayo, jambo hili linatishia uthabiti wa miradi
ya uzalishaji wa siku zijazo ambayo tayari inaendelea kujengwa.
Baada
ya zaidi ya miaka 20 ya ujenzi, EAPP, SAPP, Benki ya Maendeleo ya
Afrika, Benki ya Maendeleo ya China na Benki ya Dunia pamoja na wabia wa
sekta ya umma nchini Uhabeshi, Kenya, Zambia, Tanzania, Msumbiji,
Zimbabwe na Afrika Kusini zinaanza kuonyesha mafanikio ambayo hatimaye
yanaweza kuwa mwisho wa matatizo ya usambazaji.
Miradi
hii inaweza kuwa mwanzo wa fursa za ajabu kwa Afrika Mashariki na
Kusini, ikikuza kila kitu kuanzia usambazaji wa umeme katika miji hadi
ukuaji wa viwanda. Matokeo haya yatapatikana tu ikiwa nchi hizi zinaweza
kutumia hadi upeo uwezo wa watengenezaji na watasinia wanaoepuka kwa
hali wakitafuta kunufaika na kanda za uhamishaji ambazo zinaendelea
kukua kwa sasa.
Unafaa
kuona tu kile Umoja wa Falme za Kiarabu zimetimiza ili uone vile
uchumi unaotegemea rasilimali unaweza kubadilisha utajiri wa nchi ikiwa
uwekezaji unaofaa katika muundo msingi unafanywa. Kwa upande mwingine,
kuna mifano ambapo uwekezaji huu muhimu haukufanywa - na basi
kusababisha ghasia za kijamii.
Swali
basi ni hili - ni rais yupi atakabiliana na changamoto hii na aunde
urithi kwenye bara hili unaosoma, "Nilileta umeme barani Afrika,
nilileta mabadiliko?"
EnergyNet,
kama ilivyokuwa ikifanya kwa miaka 17 iliyopita, itarahisisha
majadiliano haya kwa kukaribisha waamuzi 100 muhimu nchini Kenya kuanzia
tarehe 25-27 Machi kwa mkutano wa Kusambaza Umeme Afrika Mashariki (http://www.powering-eastafrica.com).
DFI kuu, waendelezaji uzalishaji wa umeme na makampuni ya usambazaji
yatakuja pamoja ili kushawishi mazungumzo, wakiwezesha washiriki kuelewa
kinachoendelea katika mtandao wa usambazaji wa Afrika Mashariki kati ya
muda mfupi na muda mrefu. Kwa maelezo zaidi, tembelea www.powering-eastafrica.com
SOURCE
EnergyNet Ltd.