Monu Singh akipokea zawadi ya ushindi kutoka kwa kaptein wa timu ya Gkmkana Golf club, Robby Chadha |
Aliyekuwa
mchezaji wa timu ya Taifa wa mchezo wa Hocky nchini kwa zaidi ya miaka 10 amefanikiwa kutwaa ushindi wa jumla wa mchezo wa gofu katika mashindano
ya mwezi wa kwanza wa kuwania vikombe vya
Gupta (Gupta golf January monthly Mug) yaliyofanyika katika uwanja wa Gymkana jijini
Arusha.
Monu Singh
amefanikiwa kutwaa ushindi wa jumla wa mashindano hayo yaliyodhamini wa campuni
ya ya Gupta outo spare yalishirikisha jumla ya wanamichezo wa gofu 40 kwa kupiga mikwaju
66 katika mizunguko 18.
Katika
mashindano hayo daraja la kwanza waliocheza mizunguko 18 kila mmoja, mchezaji
Raju Lodhia alifanikiwa kutwaa nafasi ya kwanza kwa kupiga mikwaju 68
akifuatiwa na Tony Frisby kwa kupiga mikwaju 69.
Daraja la
pili ya mizunguko 18 Monu Singh alishinda nafasi ya kwanza kwa kupiga mikwaju
66, akifuatiwa na Jatin Sonecha kwa kupiga mikwaju 70, huku daraja la tatu
George Ogutu akishinda nafasi ya kwanza kwa kupiga mikwaju 73 akifuatiwa
na Jamal Mukarram aliyepiga mikwaju 74.
Aidha Abid
Ogutu alifanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwa wale waliozunguka mizunguko tisa
kwa kupiga mikwaju 33 akifuatiwa kwa karibu na Murad Jivani aliyepiga mikwaju
34 huku Jagdish Chuchu akitwaa ushindi
kwa upande wa wazee.
Akizungumzia
mashindano hayo kaptein wa timu ya Gymkana Robby Chadha alisema kuwa mashindano
hayo yaliyodhaminiwa na kampuni ya Gupta kwa miezi sita kuanzia January hadi
june yana lengo la kuboresha club ya Gymkana kwa kufanya mashindano hayo kila
wiki ya mwisho wa mwezi ambazo washindi watakuwa wanazawadiwa vikombe
mbalimbali kutoka katika kampuni hiyo.
Kwa upande
wa mshindi wa jumla, Monu Singh alisema kuwa mbali na kujiunga na club ya
mchezo wa gofu kwa miezi sita pekee lakini amefanikiwa kutwaa ubingwa wa jumla
kutokana na kucheza mchezo wa Hocky unaofanana na gofu kwa miaka 10
akiwakilisha timu ya Taifa ya Tanzania ambapo pia amekuwa akifanya mazoezi mara
kwa mara kama sehemu ya mazoezi yake.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia