Mwenyekiti
wa muda wa Chama cha Bloggers Tanzania (Tanzania Bloggers Network - TBN
), Joachim Mushi (kulia) akitoa poe na kisha kukabidhi ubani wa fedha
shilingi laki tano (500,000/-) jana zilizotolewa kwa mwanahabari wa
Kitulo FM ya Njombe Bw. Conrad Mpila kama pole toka TBN baada ya
kupoteza ndugu watano wa familia moja katika ajali ya moto iliyotokea
hivi karibuni na kuua watu sita eneo la Kipunguni jijini Dar es Salaam.
Katikati ni mmoja wa wajumbe wa TBN, Dotto Mwaibale. TBN ilishiriki
katika mazishi ya marehemu hao sita waliozikwa jana katika makaburi ya
Airwing, Dar es Salaam. Picha na Francis Dande.
"Tupo
nawe katika wakati huu mgumu..." anasema Mwenyekiti wa muda wa Chama
cha Bloggers Tanzania (Tanzania Bloggers Network - TBN ) Bw. Joachim
Mushi wakati anakabidhi ubani huo
"Pole sana Conrad", Bw Mushi anamfariji mfiwa.
habari picha kwa hisani ya TBN